BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHANZO CHA KUNYANYASWA WAANDISHI WA HABARI CHAELEZWA NA WAZIRI DK MWAKYEMBE MWANZA

Waandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd mkoa wa Morogoro, Juma Mtanda, Hamida Shariff na Habiba Yahya wakifurahia jambo muda mfupi kabla ya kuanza kwa maandano kuadhimisha kilele cha siku ya vyombo vya habari duniani yaliyoanzia Shan na kuishia Savoy leo.


WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe amesema mjadala kuhusu waandishi kunyanyaswa duniani na mazingira hasi katika baadhi ya nchi unatokana na ukosefu wa misingi imara ya kikatiba na kisheria ya kulinda uhuru wa kutafuta, kupata au kupokea na kusambaza habari.

Akizungumza leo katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari dunia zilizofanyika kitaifa mkoani Mwanza, amesema sababu nyingine za kujitokeza kwa mjadala huo ni uelewa unaopishana katika jamii kutambua na kuthamini wajibu adhimu walionao waandishi wa habari katika kuhabarisha, kuelimisha, na hivyo kufanikisha utekelezaji wa dhana ya kikatiba ya uwajibikaji wa serikali kwa umma.

Dk.Mwakyembe ametaja sababu nyingine kuwa ni vyombo vya habari kutawaliwa na msukumo mkubwa wa kibiashara lakini bila kuzingatia weledi na hivyo vingi vinategemea huduma ya ‘cheap labour’ kujiendesha na sera za uhariri za baadhi ya vyombo vya habari kukataa dhana ya mipaka ya uhuru wa habari na hivyo kujiingiza kwenye mivutano isiyoisha na Serikali na waathirika wa uhuru huo usio na mipaka.

“Hali hii inaigusa Tanzania katika maeneo kadhaa lakini je, na sisi tuna tatizo la kukosa misingi imara ya kikatiba na kisheria ya kulinda uhuru wa habari? Alihoji.

Dk.Mwakyembe alisema Ibara ya 18(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inasema kila mtu anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi.

“Ukiisoma ibara hii peke yake, unauona uhuru usio na kigugumizi wala mipaka, lakini tafsiri sahihi ya Katiba ni tafsiri oanishi (harmonious interpretation) inayosema "kifungu chochote kile cha Katiba ni sehemu ya vifungu kadhaa vinavyohusiana ambavyo ni kwa kuviangalia kwa pamoja, utapata maudhui ya kila kipengele".alisema.

Alisema waandishi wa habari wana wajibu wa kuheshimu haki na uhuru wa wengine na maslahi ya Taifa kwani ndo mpaka pekee muhimu wa kuzingatia wanahabari na watangazaji, na mpaka huu hauko Tanzania tu, ni universal.

Aliongeza kuwa waandishi na watangazaji wanapovuka mpaka huo kwa makusudi, tena bila kuomba radhi kama uungwana unavyodai pale tunapoandika au kutangaza uvumi usio wa kweli, ndivyo tunavyojenga uhasama na watu ambao hawakustahili kujenga uhasama na vyombo vya habari. 


“Kalamu yako mwandishi wa habari ina nguvu ya pekee: inajenga, inabomoa. Kalamu yako inapotetea chenye haki, uwe na uhakika kuwa baraka za wengi ziko nawe, na kwa kuwa sauti ya wengi ni sauti ya Mungu (vox populi vox Dei), una baraka na ulinzi wa Mungu,’alisema.NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: