BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAALIM SEIF HAMAD AIPA PRESHA CCM VISIWANI ZANZIBAR


KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amesema ataacha kugombea urais visiwani Zanzibar iwapo tu wananchi wataamua asigombee.

Maalim Seif tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini mwaka 1990 amegombea urais wa Zanzibar mara tano kupitia CUF na mara zote amekuwa akishindwa ingawa amekuwa akisisitiza kuwa anashinda lakini anaporwa ushindi.

“Inapofika wakati wa uchaguzi mkuu napata shinikizo kubwa la wananchi visiwani Zanzibara na bara wakitaka nigombee urais na wengine wanaamua kutoa pesa zao kunichukulia fomu ya urais,”alisema.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mahojiano na kituo kimoja cha luninga, alisema mipango ya uchaguzi mkuu wa 2020 itaanza ndani ya chama baada ya kumalizika kwa kesi iliyopo mahakamani inayohusiana na mgogoro unaoendelea katika chama.

Maalim Seif amesema pamoja na kuwepo kwa mgogoro huo, hata hivyo hakuna mgawanyiko wowote wa wanachama uliojitokeza kiasi cha kufanya kuwa na makundi mawili kwa maana ya CUF Maalim Seif na Cuf Lipumba bali ipo CUF moja ambayo ni ya wanachama. 


Kuhusu utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano, alisema yapo mambo mazuri yanayofanywa na Rais John Magufuli na yapo mengine yenye kasoro.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: