Shirika la nyumba la taifa (NHC) linatarajia kukusanya kiasi cha Sh2.84 bil baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miradi yake mipya miwili ukiwemo wa ghorofa tano na mradi wa nyumba 42 za kisasa katika mkoa wa Morogoro.
Fedha hizo zitatokana na uuzwaji wa nyumba 42 zilizopo Dakawa Mvomero huku nyumba hizo zikiwa zimeuzwa kati ya sh46 mil na sh47 mil wakati mradi wa jengo la ghorofa tano la kupangisha likitarajia kuingiza kiasi cha sh97 mil kwa mwezi.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi mipya ya NHC mkoani hapa eneo la Dakawa Mvomero, Mwenyekiti wa bodi mpya ya wakurugenzi wa shirika hilo, Blandina Nyoni alieleza kuwa hiyo ni hatua nzuri na jambo la kupongezwa.
Bodi hiyo ipo katika ziara ya kukagua miradi ya shirika la nyumba la taifa (NHC) kwa mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida.
Blandina alieleza kuwa bodi mpya imefurahishwa kuona jengo jipya la ghorofa tano ambalo litapangishwa kwa wateja lakini kuvutiwa na mradi wa ujenzi wa nyumba 42 za kisasa za Dakawa Mvomero.
“Hii ni hatua nzuri kuona miradi yenye tija na manufaa ya shirika lakini na taifa kiujumla na tutajaribu kuona nyumba zitakazojengwa baadaye kwa ajili ya kuuzwa zinauzwa kwa bei na mtanzania wa kawaida ili aweze kumudu kununua.”alieleza Blandina.
Jambo lililopo mbele yetu ni kuona shirika linatafuta teknolojia na malighafi ya bei nafuu ili kuweza kujenga nyumba zenye bei nafuu zitakazo gharimu kati ya sh20 mil hadi sh30 mil ili kuepuka bei kubwa.aliongeza Blandina.
Kwa upande wa Meneja wa shirika la nyumba la taifa (NHC) mkoa wa Morogoro, Veneranda Seiff aliwaeleza wajumbe wa bodi hiyo kuwa katika mradi wa ujenzi wa ghorofa tano lililopo katikati ya Manispaa hiyo watakusanya kiasi cha sh97 mil kwa mwezi na kwa mwaka watavuna kiasi cha sh116.4 bil.
“jengo letu la gholofa tano tunatarajia kukusanya kiasi cha sh116.4 bil kwa mwaka na mwezi tutaingiza kiasi cha sh97 mil na mpaka sasa tayari tumepokea maombi ya wapangaji wasiopungua 200.” alieleza Veneranda.
Veneranda alieleza kuwa katika mradi wa ujenzi wa nyumba 42 za Dakawa Mvomero, nyumba hizo zipo kwenye madaraja matatu tofauti zikiwa na bei kati ya sh46 mil na sh47 mil na tayari zimenunuliwa na halmashauri ya wilaya ya Mvomero isipokuwa nyumba mbili. Mkurugenzi mkuu wa shirika la nyumba la taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza jambo mbele ya wajumbe wa bodi mpya ya shirika hilo walipofanya ziara mkoa wa Morogoro kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo eneo la mradi wa nyumba 42 za Dakawa Mvomero.PICHA/JUMA MTANDA.
Mkurugrnzi mkuu wa shirikala hilo, Nehemia Mchechu aliwaeleza wajumbe wa bodi hiyo mpya kuwa changamoto wanayokumbana nayo ni upatikanaji wa viwanja kutoka halmashauri hapa nchini.
“Tunaishukuru halmashauri ya wilaya ya Mvoero kwa kutoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizi 42 lakini changamoto iliyopo mbele yetu tumekuwa tukipewa maeneo ya mbali inayoleta shida kwa huduma za kijamii kama maji, umeme hata usafiri nao unakuwa kero.”alieleza Mchechu.
Miradi ya maendeleo katika halmashauri mpya yatahitajika kuonwa na wawekezaji wengine ili kutoa nafasi ya kuwashawishi kuwekeza lakini kama miradi ya maendeleo yatafichwa basi maendeleo eneo hilo yatachelewa.
0 comments:
Post a Comment