Taarifa iliyosomwa leo na mwakilishi wa mkurugenzi wa WHO nchini, Neema Kileo inaonyesha kuwa watu 146,000 wenye umri chini ya miaka 30 hufariki dunia barani Afrika kutokana na magonjwa yanayotokana na matumizi ya tumbaku.
"Magonjwa yanayouwa zaidi kutokana na matumizi ya tumbaku ni pamoja na saratani ya mapafu, kisukari, magonjwa sugu ya mapafu, kuzaa watoto njiti, na kuharibika kwa mimba kwa mama mjamzito" amesema Kileo
Pia amesema watu 600,000 ambao si watumiaji wa sigara hufariki dunia kila mwaka kutokana na kuvuta moshi wa sigara kutoka kwa wavutaji wa sigara./Mwananchi
0 comments:
Post a Comment