DK JOHN MAGUFULI ANAPASWA KUENDELEA KUTAWALA MIAKA YOTE KAMA RAIS WA TANZANIA
Rais Dk John Magufuli akisikiliza jambo kutoka kwa Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi katika picha ya maktaba.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amesema kama si utawala wa katiba uliopo nchini, utawala wa Rais John Magufuli ulipaswa kuendelea kuwepo miaka yote.
Mwinyi ameyasema hayo leo, wakati akitoa salam za Eid El Fitr katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Amesema anayoyafanya Rais Magufuli ni mambo mazuri na kwamba kwa kiasi kikubwa amefanikiwa kulipeleka taifa mahali kuzuri.
"Amelipeleka taifa mahali kuzuri, amerudisha nidhamu, sasa hivi ukienda hospitali unapata huduma vizuri, ukienda kwenye ofisi unapata huduma nzur," amesema. "Yako mengi mazuri, tumuunge mkono Rais wetu, kama isingekuwa katika basi ningesema aendelee kuongoza mpaka mwisho." ameongeza Alhaji Ali Hassan Mwinyi.
0 comments:
Post a Comment