BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

FURAHA YA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU KATIKA SIKUKUU YA EID EL FITR 2017.

 
MTANDA BLOG inapenda na kuwatakia sikukuu njema ya sikukuu ya Eid El Fitr waumini wa dini ya kiislamu na wananchi wote, inayotarajia kusherehekewa mara baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani.

Sikukuu ya Eid El Fitr iwe yenye amani, upendo na kuwajali masikini. 

ELIMU KWA WAUMINI WA DINI YA KIISLAM.
Kabla ya kuswaliwa kwa ibada ya Eid El Fitr, mwislamu anapaswa kutoa Zaakatul-Fitr lakini endapo atatoa Zaakatul Fitr baada ya swala ya Eid El Fitr kuhesabika umetoa sadaka kama sadaka nyingine lakini ni wajibu wa kila muislam kutoa zaakatul Fitr.


Jambo lingine linalompasa muumini wa dini ya kiislamu kabla ya swala ya Eid El Fitr inamlazimu baba ama mama katika familia kuwa na jukumu la kuwatolea Zaakatul Fitr familia yake.

Mgeni ama mtoto aliyezaliwa kabla ya swala ya Eid El Fitr wanapaswa kutolewa Zaakatul Fitr na mkuu wa familia, kama mkuu wa familia ana watu 10 wanaomtegemea basi anapaswa kuwatolea Zaakatul Fitr kwa kutoa chakula kinachopendwa zaidi na watu wanaoshi eneo hilo ama mji.

Mtu mmoja anapaswa kutoa zaakatul Fitr vibaba viwili na nusu tu, mfano kama utahitaji kutoa mchele basi hesabu yake ni sawa na kilo mbili na nusu (Kg2.5) lakini ni vizuri kuonana na kiongozi wa dini ya kiislamu kwa ufafanuzi zaidi.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: