Hatimaye Mahakama Kuu ya Uganda yatoa amri kaburi la Ivan Ssemwanga, yule mtalaka wa Zari, ambaye ni mke wa sasa Diamond Platinumz 'Chibu' lifukuliwe, ili mamilioni ya pesa alizozikwa nazo zitolewe.
Mahakama imesema imechukua uamuzi huo ili kulinda heshima ya fedha ya nchi hiyo anaandika Benjamin Kasenyenda Andongolile.
Mahakama imechukua uamuzi huo baada ya Mganda mmoja aitwaye Mgugu Abey, kuwashtaki Mahakamani kampuni iliyoraribu mazishi hayo ya A Plus Funeral Management na Benki Kuu ya Uganda,ambayo imeonekana ilizembea kwenye tukio hilo.

Hivyo, mahakama imeamuru kampuni ivunje kaburi kwa gharama zao,ili mlalamikaji achukue pesa hizo kwa niaba ya mataifa yenye fedha hizo, kwani zilikuwepo Rand za Afrika Kusini,Dola za Marekani pamoja na Shilingi za Uganda.
Kisha kampuni ya A Plus imeamriwa ilifukie kaburi hilo kwa gharama zake na kisha kumlipa ndugu Abey gharama zingine za usumbufu.Nakala ya huku inaletwa
Ama kweli mjini shule.
0 comments:
Post a Comment