VIPODOZI VYA VYA SUMU CHANZO CHA UGONJWA WA SARATANI YA NGOZI, UBONGO NA FIGOvipodozi vya sumu
Saratani ya ngozi, ubongo, ini na figo ni matokeo ya vyakula vilivyoisha muda wa matumizi na vipodozi vyenye viambata vya sumu.
Akizungumza wakati wa uteketezaji wa bidhaa hizo, Mfamasia wa TFDA Manispaa ya Sumbawanga, Fortunata Kumbakumba, alisema madhara mengine ni mjamzito kuzaa mtoto mwenye utindio wa ubongo, wanawake kuwa hatarini kuota ndevu na wanaume matiti.
Awali, Mkaguzi Mwandamizi wa TFDA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Yola Hudege alisema bidhaa za chakula, dawa za matumizi ya binadamu na vipodozi vyenye viambata vya sumu zenye thamani ya Sh4.5 milioni vimeteketezwa.
Mratibu wa TFDA Manispaa ya Sumbawanga, Ally Lubeba alisema wanaendelea kuchukua hatua za kisheria kupambana na wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa hizo sokoni.Mwananchi
0 comments:
Post a Comment