Kasuku sawa na huyu ana uwezo mkubwa wa kuiga sauti
Mwanamke amepatikana na hatia ya kumuua kwa kuimpiga risasi mumewe mara tano katika jimbo la Michigan kwenye kisa ambacho kilishuhudiwa na kasuku.
Glenna Duram alimpiga risasi mumewe mbele ya kasuku huyo mwaka 2015 na kisha akajaribu kujiua kwa kujipiga risasi.
Kasuku huyo anayejulikana kama Bud, baadaye alirejelea maneno "usipige risasi" kwa sauti ya muathiriwa, kwa mujibu wa mke wa zamani wa Duram. Glenna Duram amepatikana na hatia ya kumuua mumewe Martin
Hata hivyo kasuku huyo hakutumiwa wakati wa kesi mahakamani.
Jaji alimpata Bi Duram 49, na makosa wa mauaji na atahukiwa mwezi ujao.
Alipata majeraha ya kichwa wakati wa kisa hicho kilichotokea nyumbani kwao mwezi Mei mwaka 2015.
Mke wa zamani wa Duram Christina Keller, ambaye sasa anamiliki Kasuku Bud, mapema alisema anaamini chiriku huyo alikuwa akirejelea mazungumzo ya kutoka usiku wa mauaji ambayo anasema yaliishia kwa kusema "usipige risasi".BBC
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kimataifa /
slider
/ KASUKU AFICHUA MAUAJI BAADA YA MWANAMKE KUMUUA MUMEWE KWA KUMPIGA RISASI
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment