BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

OFISI YA MWANASHERIA MKUU YAMTAKA MKUU WA JESHI LA POLISI KUTOA MAELEZO JUU YA MATUMIZI YA NGUVU DHIDI YA RAIA

Ofisi ya mwanasheria mkuu nchini Venezuela imemtaka mkuu wa zamani wa jeshi la polisi kutoa maelezo juu ya matumizi ya nguvu zilizopitiliza dhidi ya mamizi ya waandamanaji wanaoipinga serikali nchini humo.

Ofisi hiyo imesema kuwa kuna ushahidi wa kutosha juu ya matumizi ya nguvu zilizopitiliza kwa waandamanaji.

Antonio Benavides anatarajiwa kuhojiwa siku Julai sita.

Aliondolewa madarakani wiki iliyopita, baada ya polisi aliowapa maelekezo kuonekana wakiwafyatulia risasi waandamanaji.

Zaidi ya watu 80 wameuawa katika maandamano ya miezi mitatu ya kupinga utawala wa Rais Nicolas Maduro.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: