BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RPC AKABIDHI UKAMANDA WA JESHI LA POLISI KWA WENYEVITI WA SERIKALI YA MITAA MOROGORO

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei.

Juma Mtanda, Morogoro.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amejivua cheo chake na kukikabidhi kwa wenyeviti wa serikali za mitaa huku mmoja wa wenyekiti hao akizima tukio la ubakaji mkoani hapa.

Akizungumza na wenyeviti wa serikali za mitaa Manispaa ya Morogoro katika Bwalo la Umwema la JWTZ mjini hapa, Matei alisema kuwa ameukabidhi ukamanda wa polisi kwa wenyeviti wa serikali ya mitaa ili waweze kutekeleza majukumu ya kipolisi kwa ngazi ya mtaa.

Matei alisema kuwa lengo hilo ni kwa ajili ya kudhibiti matukio ya kiuhalifu na kusimamia vyema kazi ya ulinzi na usalama ikiwemo kuwabaini wahalifu na kuwakamata kwa njia ya usalama bila kuwajeruhi.

“Nitabakia kuwa kamanda wa polisi ngazi ya mkoa lakini kwa ngazi ya mtaa ninyi wenyeviti wa serikali ya mtaa ndio mtakuwa makamanda ili mtekeleze vyema kazi za ulinzi na usalama maana mmetajwa katika katiba mkasimamie vizuri kazi ya ulinzi na usalama lakini na mchunguze nyendo za kila watu wanaoishi mtaani na mdhibiti.”alisema Matei.

Matei aliongeza kwa kusema kuwa kazi yao hao viongozi watashirikiana na mabalozi wa nyumba kumi kumi kwa kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi ili kuendesha shughuli za ulinzi ndani ya mitaa yao.

“Ulinzi shirikishi ni mzuri kwani ninatumaini mtaweza kukamata wahalifu wa madawa ya kulevya, kubaini matukio yanayopangwa na kuvuruga mipango ya wahalifu na kuwakamata katika ukamataji salama ili watuhumiwa wafikishwe kituoni wakiwa salama.”alisema Matei.

Kwa upande wa wenyeviti hao, walieleza kufurahishwa na kitendo cha kamanda Ulrich Matei kuandaa mafunzo mafupi ya namna ya kubaini matukio na kuyazima kupitia ulinzi shirikishi yakihusisha wenyeviti wa serikali za mitaa ndani ya Manispaa ya Morogoro.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kihonda B, Auleria Mbeye alieleza kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara ili kuweza kuwatia hatiani watuhumiwa wanaotenda makosa ya aina mbalimbali.

Auleria alisema kuwa hajui namna ya kumtia hatiani kwa mtu mwenye mipango ya kutekeleza tukio la ubakaji.

“Tulifanikiwa kuzima tukio la mtoto wa kike kutaka kubakwa na mmoja wa mwanaume katika mtaa wetu lakini baada ya kumkamata na kufikishwa polisi aliweza kuachiwa baada ya wiki moja lakini kama tungepata mbinu nzuri mtaa wetu ungekuwa wa kuogopewa na wahalifu wa kila aina.”alisema Auleria.

Katika mtaa wa Mgaza kata ya Mindu umetajwa kuwa moja ya mitaa yenye maficho ya wahalifu hasa baada ya kufanya matukio mbalimbali ndani ya Manispaa hiyo.

Mwenyekiti wa serikali ya Mgaza, Jumanne Matipa alieleza kuwa mtaa wake umekuwa kimbilio la wahalifu hivyo kuomba jeshi la polisi kumuongezea nguvu ya kupambana nao na kuwatia nguvuni.

Kamanda wa polisi wa mkoa huo amelazimika kuwaita wenyeviti wa serikali za mitaa Manispaa ya Morogoro ili kuwaongezea ujuzi wa namna ya kukabiliana na matukio ya uhalifu na ukamataji salama kwa watuhumiwa bila kuwajeruhi kupitia ulinzi shirikishi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: