BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

USHAURI KWA CHADEMA KUHUSU TUNDU LISSU ASIACHWE PEKEE YAKE





Image may contain: 2 people, people standing Rais wa 36 wa Marekani, Lyndon Johnson alikuwa akimuogopa mwanaharakati mwanamke wa Mississippi, Fannie Lou Hamer kuliko Martin Luther King Jr.

Ni kwa nini? Sababu ni kuwa Hamer alikuwa mbwatukaji. Alipowekwa mahabusu na kupigwa, alipoachiwa alitokeza mbele ya vyombo vya habari na kueleza kila alichofanyiwa.

King yeye alikuwa mjenga hoja za kuelimisha kuhusu usawa, hakuwa mwingi wa maneno yenye kuwaudhi watawala, lakini Hamer alipozunguza, watawala walikunja ndita.

Ndiyo maana King aliweza kuzungumza na Rais Johnson akabaki kimya, lakini Hamer alipotoa hotuba zake, ilibidi Rais Johnson azijibu. Ni kwamba hoja za Hamer zilikuwa kali na zenye kuhamasisha hisia za chuki kwa Wamarekani Weusi dhidi watawala.

Ujasiri mkubwa wa Hamer ulitokana na nini? Jawabu lipo kwenye neno moja; watu.

Ndiyo, watu ndiyo waliokuwa wakimpa Hamer kiburi cha kupambana na kusema jambo lolote aliloona linafaa kusemwa hata kama ilikuwa hatari kwake. Hamer alipokamatwa, alijua ana watu nje waliompigania atoke.

Na kweli, Hamer aliwaona watu akiwa mahabusu, hata alipozuiwa kuonwa, alipata taarifa kuhusu watu kumpigania. Alipoachiwa, alipokelewa na watu kwa furaha na kumfariji.

Ieleweke kuwa watu ndiyo nguvu na faraja kwa mwanaharakati. Ukitaka mwanaharakati astaafu mapema ni pale anapoingia kwenye matatizo na dola halafu ajikute peke yake.

Kwa lugha nyoofu ni kuwa mwanaharakati nguvu yake ni watu wakweli wanaomuunga mkono na kumpigania bila kujali chochote. Sumu ya mwanaharakati ni watu wanafiki, wanaomtenga pale mambo yanapokuwa magumu.

Wamarekani Weusi wamekuwa na mafanikio Marekani katika vita ya ubaguzi wa rangi kwa sababu ya kutokuwa wanafiki. Afrika Kusini akina Nelson Mandela waliwashinda makaburu kwa sababu ya kutokuwa wanafiki.

Mandela angelainika na kukata tamaa kama angejiona yupo peke yake. Hata hivyo, alivumilia mateso ya miaka 27 jela kwa sababu alikuwa na watu. Akiwa jela, alijua watu walipigana kwa ajili yake na Waafrika Kusini Weusi wote. Alijua Afrika ilimlilia, hivyo hakuwa na sababu ya kukata tamaa.

Chadema wanapaswa kuwa wakweli bila chembe ya unafiki kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu. Wanapaswa kumnyima sababu ya kukata tamaa.

Kuna mawili; kama Chadema hawaamini katika kile ambacho Lissu anakifanya mpaka anaingia kwenye matatizo na dola, basi wakae naye chini na kumshauri aache. Ikiwa wanakiamini na wanaunga mkono, basi wawe naye bega kwa bega wakati wote.

Siku Lissu atakapojikuta peke yake ndiyo utakuwa mwanzo wa kukata tamaa. Utakuwa mwanzo wa kuchoka na kuvunjika moyo. Angalau sasa anawaona akina Fatma Karume, Peter Kibatala na wengine wapo naye. Hao ndiyo wanampa nguvu na ujasiri wa kuendelea.

Hili si kwa Lissu tu. Inamhusu Godbless Lema na wengine wote. Harakati sumu yake ni kutengwa na watu unaoamini upo nao. Kuna wanaharakati walikuwa moto ila sasa wamepoa.

Huwezi kujua ni yapi yenye kuwaumiza moyoni. Walivunjika moyo kiasi gani walipotengwa na walioamini wapo nao!

Mtu anapojilipua maana yake anaamini kuna watu yupo nao ila yeye anajiweka mbele kwa maslahi ya wengi. Sasa ajilipue halafu atengwe. Unaweza kukuta anabadili uelekeo wa harakati zake na kuanza kupambana ndani ya chama chake. Ni hapo chama kitakuwa hatarini kwa mpasuko.

Ni ushauri wa Kiswahili ambayo ni lugha yetu rasmi Watanzania, hivyo nimeeleweka. Ushauri uwekwe akilini, Ndimi Luqman MALOTO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: