MBUNGE wa Itilima mkoani Simiyu, Njalu Slanga, amewaomba wazee wa mila katika vijiji vinavyopakana na Pori la Akiba la Maswa kutumia njia za mila katika kupambana na tembo wanaotoka katika pori hilo.
Slanga alisema zamani wazee wa mila walikuwa wakitumia njia hizo kupambana na wanyama hao wanapovamia mazao na nyumba zao, bila a kuwapo madhara kati yao na wanyama hao.
Mbunge huyo alikuwa alitoa kauli hiyo katika Kata ya Logalombogo baada ya wananchi kumweleza kuwa tembo wamekuwa kero kubwa kwao na familia zao.
Walisema wamekuwa wakilazimika kulala mapema kwa kuogopa kukutana na wanayama hao na kusababisha kuishi kwa hofu kila siku.
“Tembo hawa wamesababisha sisi kuishi kwa hofu, kila mwaka kwetu ni njaa kutokana na mazao yetu kuharibiwa na wananayama hawa.
“Hiki kilimo kimekuwa cha muda mrefu, sijui mnataka na sisi tuchukue uamuzi mgumu?” alisema Maria Manyangu.
Mbunge huyo aliwataka wananchi hao wasichukue uamuzi wa kuwaua tembo hao.
Aliwaomba wazee kutumia njia za mila kuzuia wanyama hao wasifanye uharibifu huo.
Vilevile alisema atalifanyia kazi tatizo la wanyama hao kwa kuomba kijengwe kituo cha askari wa wanayama pori katika vijiji vilivyoko kwenye kata hiyo kuzuia maafa yanayosababishwa na wanyama hao.
“Wakati mimi naendelea kupambana kuletwa vituo vya askari kwenye kata hii, wazee nawaomba tutumie zile njia za zamani, mbona uko nyuma tulikuwa tunafanikiwa na hawa wanyama wanarudi kwenye pori?
“Hakuna madhara kwetu hata kwa wanyama wenyewe,” alisema Njalu.MTANZANIA
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
slider
/ MBUNGE AWASHAURI WANANCHI KUPAMBANA NA TEMBO WANAOVAMIA MASHAMBA NA KUTISHIA MAISHA KUWAFUKUZA KUTUMIA NJIA ZA ASILI
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment