Wanawake nchini Saudi Arabia wameruhusiwa kuendesha magari kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo.
Uamuzi huo wa Mfalme Salman utaanza kutekelezwa kuanzia Juni 2018, ambapo wanawake watakuwa na haki sawa na wanaume katika kuendesha magari.
Saudi Arabia lilikuwa Taifa pekee duniani ambalo lilikuwa halijaruhusu wanawake kuendesha magari tofauti na mataifa mengine yote ulimwenguni ambayo yanaruhusu wanawake kumiliki na kuendesha magari.
Mfalme wa Taifa hilo, Salman bin Abdulaziz Al Saud ametoa ruhusa hiyo ikiwa ni muda mfupi baada ya kiongozi maarufu wa kidini wa nchi hiyo kusema kuwa wanawake wasiruhusiwe kuendesha magari kwa kuwa umakini wao ni robo ya umakini wa wanaume.
Kwa mujibu wa tamko la Mfalme Salman, suala hilo litatekelezwa kwa kufuata taratibu na sheria za dini ya Kiislamu. Huu ni ukombozi mkubwa kwa wanawake wa Saudi Arabia ambao kwa muda mrefu wamekuwa katika marufuku ya kutoendesha gari.
Mwanamke nchini Saudi Arabia anaweza kumiliki gari lakini haruhusiwi kuliendesha badala yake anatakiwa aliendeshe mume wake.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment