Klabu ya Simba inawatangazia waandishi wote wa habari za michezo, kuwa leo 18/9/2017 kutakuwa na mkutano utafanyika kwenye ukumbi mdogo wa klabu hiyo kuanzia majira ya saa 6 mchana pamoja na mengine yatakayozungumzwa.
Mkutano huo utawakutanisha waandishi wa habari na viongozi wa Simba SC wataelezea mambo mengi ya umuhimu ya kuyatolea ufafanuzi na kuyaweka wazi kwa umma wa mashabiki na wanachama wa klabu yao kupitia vyombo vya habari.
"Tunasisitiza kuwa mkutano huo utaanza katika muda uliotajwa hapo juu na utazingatia muda."alieleza Haji Manara.
Klabu inapenda kuwapa taarifa rasmi, kuwa kuanzia sasa kila siku ya Jumatatu tu tutakuwa na mkutano kuanzia majira ya saa 6 mchana kwenye ukumbi wa klabu hivyo basi ni vyema mkaiongeza ratiba hii kwenye ratiba zenu za kazi za kila siku .
Imetolewa na Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano
Haji S. Manara.
Simba Nguvu Moja.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment