Juma Mtanda, Morogoro.
Chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo Morogoro (SUA) kimepigwa jeki na benki ya CRDB kwa kukabidhiwa hundi yenye thamani ya sh15 milioni ili kuwezesha kufanyika kwa bonanza la michezo la wafanyakazi wa chuo hicho litakalojumuisha jumla ya michezo 11 na kufanyika Oktoba 13 mwaka huu, mkoani hapa.
Wafanyakazi hao watachuana na kuonyesha vipaji katika michezo ya soka, netoboli, kuvuta kamba, Volvo, tenis, pooltable, riadha, mpira wa wavu, drafta, bao na kufukuza kuku ambapo washindi watakabidhiwa zawadi mbalimali baada ya kushinda.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hundi hiyo mkoani hapa, Mkurugenzi wa benki ya CRDB mkoa wa Morogoro, Lusingi Sitta alisema kuwa fedha hizo zitasaidia kufanikisha bonanza hilo na kutoa nafasi kwa wafanyakazi kupata fursa ya kushiriki michezo hiyo.
Sitta alisema kuwa sehemu hiyo ya fedha kwa ajili ya bonanza hilo la michezo ni mwanzo wa benki hiyo ya CRDB kurejesha fadhila kwa wateja wake na chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo ni moja ya wateja wakubwa wa siku nyingi na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo.
“Ushirikiano kati yetu sisi benki ya CRDB na chuo kikuu cha Sokoine (Sua) unadhihirika namna tunavyoshirikiana ambapo kati ya wakurugenzi 12 waliopo benki ya CRDB kati yao wakurugenzi watatu wamehitimu kozi mbalimbali ndani ya chuo kikuu hiki hivyo ni nafasi ya wafanyakazi sasa kuonyesha ujuzi wenu.”alisema Sitta.
Kwa upande wa Meneja Mikopo ya Biashara wa CRDB, Theo Madilu alisema benki yao imekuwa na historia nzuri na chuo hicho kwa kuajiri wahitimu mbalimbali wenye weledi.
Theo alisema kuwa kutokana na kufanya kazi kwa kushirikiana, kumewezesha kuanzisha huduma rafiki wakati wa zoezi la udahili wa wanafunzi na kufanikisha malipo mbalimbali ya wadahiliwa wa chuo kupitia benki ya CRDB.
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Prof Raphael Chibunda ameipongeza benki hiyo kwa kuwa mfadhili wa kwanza kufadhili bonanza lao la michezo kwa ajili ya wafanyakazi hao.
Prof Chibunda alisema kuwa chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo kimeahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa uongozi wa benki hiyo katika masuala mazima ya maendeleo ambapo kwa ushirikiano huo wakulima wadogo hususani wale wa vijijini wataweza kunufaika na utaalamu kutoka kwenye chuo hicho.
Benki ya CRDB kwa sasa inamilikiwa 100% na wazawa baada ya serikali kununua hisa zote 21 zilizokuwa zikimilikiwa na shirika la maendeleo la Dernmark (Danida).
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / michezo /
slider
/ CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA) CHAPIGWA JEKI YA SH15 MIL NA CRDB MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment