Nyumba za wabunge wa upinzani zashambuliwa
Vitu vinavyokisiwa kuwa guruneti vimetumiwa kushambulia nyumba za wabunge wawili wa upinzani nchini Uganda, mmoja wao akiwa ni mwanamuziki ambaye sasa ni mbunge Bobi Wine, kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la nchini humo.
Polisi sasa wanachunguza mashambulizi kwenye nyumba za Bobi Wine ambaye jina lake kamili ni Robert Kyagulanyi, anayewakilisha eneo la Kyaddondo West na Allan Ssewanya ambaye ni mbunge wa Makindye West.
Mashambulizi hayo yalifanyika mapema Jumanne.
Wiki iliyopita shambulizi liliripotiwa kwenye nyumba na mbunge mwingine Moses Kasibante ambaye ni mbunge wa Rubaga North.
Kwenye ujumbe kupitia mtandao wa Facebook, Bobi Wine alisema kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa nyumbani kwake
Amesema amekuwa akipokea vitisho vya kuuliwa karibu kila siku.
Gazeti la New Vision lilisema kuwa wabunge ambao nyumba zao zilishambuliwa ni badhi ya wale waliotimuliwa bungeni kufuatia ghasia wakati wa mijadala kuhusu kuondolewa kwa umri wa kuwania urais.
0 comments:
Post a Comment