BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SHEIKH PONDA ATII SHERIA BILA SHURUTI, AJISALIMISHA KITUO CHA POLISI DAR ES SALAAM

Katibu mkuu wa baraza la mashirika ya kiislamu nchini Tanzania Sheikh Issa Ponda amejisalimisha katika kituo cha polisi cha Central kufuatia agizo la kamanda mkuu wa polisi wa maeneo maalum mjini Dar es Salaam RPC, Lazaro Mambosasa.

Kiongozi huyo wa dini alimewasili katika kituo hicho cha polisi leo Ijumaa akiwa na wakili wake, Abdallah Safari.

Mambosasa alimwagiza Sheikh Ponda tangu jana kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi kutokana na matamshi ya uchochezi aliyotoa.

Kulingana na kamanda huyo , Kiongozi huyo wa dini alifanya makosa hayo siku ya Jumatano wakati wa mkutano na vyombo vya habari mjini na alitakiwa kujisalimisha kati ya Alhamisi na Jumamosi la sivyo akamatwa.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: