BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TAJIRI NAMBARI MOJA AFRIKA, ALIKO DANGOTE AONYA SERA ZA UWEKEZAJI ZA RAIS JOHN MAGUFULI TANZANIA


Tajiri namba moja barani Afrika Aliko Dangote ambaye pia ni mwekezaji mkubwa nchini Tanzania amemuonya Rais John Pombe Magufuli kuwa sera zake nchini humo zinawaogopesha wawekezaji.

Dangote ambaye amewekeza dola za kimarekani 650 kwenye uzalishaji wa saruji, amesema ni wakati umefika kwa rais Magufuli kuzipitia upya sera zake ama akubali kuingia katika hatari ya kuwapoteza wawekezaji wote nchini humo.

Rais Magufuli alipoingia madarakani, wawekezaji na wafanyabisahara walifurahishwa kwa jinsi alivyopambana na rushwa lakini miaka miwili baadae, baadhi ya wafanyabiashara wamegubikwa na hofu hasa baada ya kuona mazingira ya kibiashara yamebadilika kutokana na mfumo wake wa utawala.

Mapema mwaka huu rais Magufuli alianzisha uchunguzi wa kina katika sekta ya madini na kubaini uhalifu mkubwa ambao ulisababishwa kuundwa kwa sheria mpya ya madini.

Katika kongamano lililofanyika mjini London, mfanyabiashara huyo alisema sheria mpya zinazoundwa Tanzania zinaiweka nchi hiyo kwenye hatari ya kuwafukuza wawekezaji wote na kushindwa kuwarejesha tena.

Serikali nchini humo ina amini kwamba sheria hizo zitawanufaisha wananchi kutokana na rasilimali za taifa lao licha ya kwamba makampuni ya kigeni yamekuwa yakipinga mabadiliko hayo ya sheria kwa madai hazitekelezeki.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: