![](https://www.habarileo.co.tz/images/STEPHANE-DUJARRIC.jpg)
Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN, Stephane Dujarric
UGANDA.Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) amefariki huko Kampala, Uganda alikokuwa akipatiwa matibabu.
Marehemu ni miongoni mwa wanajeshi waliokuwemo kwenye ngome ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa (MANUSCO) iliyoshambuliwa kwa kuviziwa na waasi huko Semuliki, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kwa mujibu wa UN, askari waliofariki sasa wamefikia 15. Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN, Stephane Dujarric, ametangaza kifo cha shujaa huyo katika mkutano na wanahabari huko New York, Marekani jana.
"Misheni ya UN huko DRC (MONUSCO) imethibitisha kuwa mlinda amani wa 15 amefariki huko Kampala...." taarifa ya UN imesema.
Hata hivyo, UN imetuma salamu za rambirambi kwa ndugu wa marehemu, wananchi, serikali ya Tanzania na walinda amani wa umoja huo.
0 comments:
Post a Comment