BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ASKOFU MKUU WA KANISA LA EAGT ASIMAMISHWA KAZI BAADA KUMFUKUZA MAKAMU ASKOFU

 
Dar es salaam. Bodi ya Wadhamini ya Kanisa la Evangelistic Assemblies Of God Tanzania (EAGT) imemsimamisha Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Mchungaji Brown Mwakipesile ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

Wengine waliosimamishwa leo Desemba 18 ni Katibu Mkuu, Mchungaji Leonard Mwizarubi na Mhasibu Mkuu, Mchungaji PrayGod Mngonja.

Pamoja na mabadiliko hayo, bodi imewateua kwa muda kushika nafasi hizo, Askofu Mkuu atakuwa ni Mchungaji Asumwisye Mwaisabila, Katibu Mkuu atakuwa Dk Jakob Madaha na Mhasibu Mkuu atakuwa Andrea Salu.

Kwa mujibu wa Katiba ya EAGT ya Mwaka 2011 ,ibara ya 6(b)(5) kinatoa mamlaka Kwa Wajumbe wanne wa bodi hiyo kusimamisha viongozi wakuu wa kanisa akiwamo Askofu Mkuu kabla ya Mkutano Mkuu kujadili maazimio hayo.

"Baada ya siku 30 kuanzia leo (jana) tutakuwa na mkutano mkuu wa Kanisa kwa ajili ya kupitisha mabadiliko hayo, wamesimamishwa kwa kumfukuza Makamu Askofu Mkuu wakidai alitenda dhambi, walimfukuza uchungaji na uumini pia," ni kauli ya Mwenyekiti wa bodi hiyo, John Mfuko alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Mzee Mfuko ambaye anazungumza kwa taabu kutokana na umri wake alisema kosa la viongozi hao wa kanisa ni kumfukuza bila kushirikisha bodi ya Wadhamini.

Mzee Mfuko aliyeongozana na wajumbe wawili kati ya wanne wa bodi hiyo alisema licha ya mahakama kubatilisha suala la kumfukuza, Askofu Mkuu (aliyefukuzwa) alikataa kumrejesha kanisani. Tuhuma nyingine ni kushiriki njama za kuhujumu mali za kanisa.

Baada ya kutafutwa kwa simu yake ya mkononi, Askofu aliyesimamishwa Mwakipesile hakupatikana kwenye simu yake ya mkononi. 


Mbali na tuhuma hizo, bodi imewataka waumini wa kanisa hilo kutotuma pesa katika akaunti za kanisa huku ikiweka wazi kushikilia akaunti hizo kutoka mikononi mwa viongozi waliokuwa na dhamana ili kuhakiki wa mali za kanisa.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: