BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KLABU YA BIRDI RALLY YATWAA UBINGWA MBIO ZA MAGARI ZA MOUNT ULUGURU RALLY MOROGORO


Juma Mtanda, Morogoro.

Klabu ya Birdi Rally ya Dar es Salaam imetwaa ubingwa wa mbio za magari za Mount Uluguru 2017 baada ya kuwatimulia vumbi na kuwahenyesha wapinzani wao 15 katika mbio hizo za kilometa 164 zilizofanyika kwa mara ya kwanza katika eneo la barabara za mashamba ya Mtibwa Sugar wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.

Katika mbio hizo zilifanyika desemba 17 mwaka huu, klabu hiyo ikimtumia dereva machachari, Randeep Birdi na msaidizi wake, Zubeyr Piredina walitumia muda wa saa 1:06:04 kumaliza mbio hizo kwa mizunguko sita za kilometa za kilometa 164 wakitumia gari aina ya Mitsubishi Evolution 9.

Akizungumza mara baada ya kushinda mbio hizo, Randeep Birdi alisema kuwa amepata faraja kubwa klabu nay eye kushinda kwani haikuwa kazi rahisi kuibuka kidede mbele ya wapinzani wake wenye viwango vikubwa katika mchezo huo.

Birdi alisema anamshukuru mwenye mungu kumwezesha kumaliza salama mbio hizo na kumwepusha na changamoto ambazo zingesababisha kushindwa kumaliza nafasi hiyo ya kwanza.

“Mashindano yalijaa changamoto nyingi lakini nashukuru mwenye mungu kushinda mbio hizo na klabu yetu kutwaa ubingwan huu.”alisema Birdi.

Birdi alisema kuwa endapo atapata wadhamini yupo tayari kushiriki mashindano makubwa ya mbio za magari mwakani.

Mwenyekiti wa klabu wa mbio za Mount Uluguru Morogoro, Dk Mossi Makau alisema kuwa wanajivunia kuweka histori ya kwanza kuchezesha mashindano makubwa kwenye eneo la barabara binafsi tofauti na hapo awali wakitumia barabara za umma.

Dk Makau aliwataja washindi tatu bora kuwa ni klau ya Birdi Rally ya Dar es Salaam iliyotwaa ubingwa huo huku nafasi ya pili ikishikwa na Mkwawa Rally Iringa kupitia dereva wake Gerard Miller akisaidiwa na Peter Fox wakitumia gari aina ya Mitsubishi Evolorion 9 na kumaliza na muda wa saa 1:06:26.

Nafasi ya tatu ilienda kwa klabu ya Hari Singh Rally wakimaliza kwa muda wa saa 1:07:10 chini ya dereva Ajminder Singh na msaidizi wake Absolom Aswani wakitumia gari aina ya Subaru Impreza.

Naye Mratibu wa mbio hizo, Faheem Aloo alisema kuwa mbio hizo zilishirikisha jumla ya klabu 16 kutona ndani ya Tanzania nje na kufanyika siku mbili.

Aloo alisema kuwa siku ya kwanza madereva 15 waliingia kwenye mchezo huo wa kilometa 1.55 zikifanyika kwenye uwanja wa Tumbaku Manispaa ya Morogoro ili kukonga nyoyo za mashabiki wa mchezo huo kabla ya kuhamia eneo la barabara za mashamba ya Mtibwa Sugar wilayani Mvomero.

“Mbio za Mvomero jumla ya klabu 16 zimeshiriki lakini ni madereva 10 pekee waliofanikiwa kumaliza na magari sita yalishindwa kuendelea na mbio kutokana na kupata hitilafu kwenye gia boksi na injini na gari moja iliweza kupata ajali na kupinduka na kushindwa kuendelea.”alisema Aloo.

Madereva wote 10 waliomaliza mbio hizo walikabidhiwa zawadi ya vikombe kulingana na nafasi zao.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: