![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgxc4xYQRo-0Lnpslhw-mTiisZWTWtRd33MA1J3w7i4rHOhrEUADkGF8MVZp21qDqx6EP1833b2jW-usVmRrAlJs5n71PNtHMlaGH0M2o66zf21OqkE5FgCOei6BFe8IxADJbkuCdJaMQc/s640/MBUNGE+WA+JIMBO+LA+KILOMBERO+PETER+LIJUALIKALI+NA+SUZAN+KIWANGA+PIX+NO+2.jpg)
Juma Mtanda, Morogoro.
Mbunge wa jimbo la Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali ameachiwa kwa dhamana baada ya kukamatwa na maofisa wa polisi muda mfupi baada ya kughairishwa kwa mashtaka yeye na wenza 56 jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro.
Kabla ya kuachiwa kwa dhamana, Lijualikali ambaye anakabiliwa na kesi iliyoko mahakamani ya ushawishi na kuchoma moto ofisi ya serikali ya kijiji cha Sofi Malinyi amehojiwa kwa saa kadhaa katika kituo cha polisi mkoani Morogoro baada ya kukamatwa jana.
Akieleza sababu zilizopelekea kukamatwa kwa mbunge huyo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema anatuhumiwa kwa kosa la kimtandao ambalo ni kusambaza picha za mtu anayedai kuwa anataka kumuua jambo ambalo ni kosa kisheria.
Kamanda Matei alisema kuwa baada ya kuhojiwa kwa kina wameamua kumuachia kwa dhamana hata hivyo uchunguzi zaidi unaendelea kuhusiana na tuhuma hizo na upo uwezekano wa kumfikisha mahakamani baada ya kukamilika kwa uchunguzi.
Mbunge Peter Lijualikali, Suzan Kiwanga ambaye ni mbunge wa jimbo la Mlimba na wenzao 55 jana walifika katika mahakama ya hakimu mkazi Morogoro wanashtakiwa kwa makosa nane.
Moja ya makosa hayo limo la kuchoma moto ofisi ya kijiji cha Sofi Malinyi Oktoba 26 mwaka huu yanayodaiwa kufanywa na watuhumiwa hao baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa marudio wa udiwani kata hiyo.
0 comments:
Post a Comment