BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MIILI YA WANAJESHI 14 WA TANZANIA WA UMOJA WA MATAIFA YAWASIRI DAR ES SALAAM


Miili ya wanajeshi 14 wa Tanzania waliouawa wakihudumu katika kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewasili jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Miili hiyo imesafirishwa kwa ndege za Umoja wa Mataifa kutoka nchini DR Congo.

Waliuawa wakati wa shambulio lililotekelezwa Alhamisi jioni kwenye kambi ya jeshi ya Semuliki eneo la Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Wanajeshi wengine zaidi ya 50 walijeruhiwa.

Umoja wa Mataifa ulisema wanajeshi 5 wa jeshi la DR Congo (FARDC) waliuawa pia kwenye shambulio hilo.

Waasi wa ADF ndio wanaotuhumiwa kutekeleza shambulio hilo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alishutumu vikali shambulio hilo na kusema ni sawa na uhalifu wa kivita. Miili ikitolewa kwenye ndege na wanajeshi

Aliitaka DR Congo kufanya uchunguzi kuhusu shambulio hilo na kusema kwamba waliohusika wanafaa kuwajibishwa.

Wanajeshi zaidi walitumwa eneo hilo na kamanda wa kikosi cha kulinda amani anaelekeza shughuli ya kuwaondoa majeruhi.

Guterres alisema shambulio hilo ndilo mbaya zaidi kuwahi kutekelezwa dhidi ya walinda amani wa UN katika historia yake miaka ya karibuni.Maafisa wakuu wa jeshi walikuwa uwanja wa ndege kuilaki miili hiyo
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: