![Shyma appears in the video for I Have Issues](https://ichef-1.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/77FA/production/_98841703_mediaitem98841699.jpg)
Shaimaa Ahmed, 25, ambaye kimuziki anafahamika kama Shyma, alikamatwa mwezi uliopita baada ya video hiyo kuzua ghadhabu kwenye taifa hilo.
Siku ya Jumanne alipatikana na hatia ya kuunga mkono mapenzi na kwa kuchapisha video inayokiuka maadili.
Mwelekezi wa video pia naye alihukumiwa kifunga cha miaka miwili licha ya yeye kutowepo mahakamani.
Shyma alikuwa ameomba msamaha kabla ya kukamatwa kwake.
"Sikufikiria haya yote yatafanyika na kwamba ningeshambuliwa kwa njia hii kali kutoka kwa kila mtu."
Mwaka uliopita mahakama nchini Misri ilawahukumu wacheza dansi watatu wanawake miezi sita gerezani baada ya kuwatuhumu kwa kuchochea ngono kwenye video ya muziki.
Mwimbaji mwingine anakabaliwa na kesi kwa kueneza uvumi kuwa maji ya mto Nile yanaweza kumfanya awe mgonjwa.BBC
0 comments:
Post a Comment