BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TAKUKURU YAMPANDISHA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA (UVCCM) KIZIMBANI MAHAKAMA YA DODOMA KWA TUHUMA ZA RUSHWA


Dodoma. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Dodoma imemfikisha mahakamani aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Sadifa Juma Khamis.

Sadifa ambaye pia ni mbunge wa Donge, Zanzibar amefikishwa leo Jumatatu Desemba 11,2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma kwa makosa mawili.

Kamanda wa Takukuru mkoani Dodoma, Emma Kuhanga alisema jana Jumapili Desemba 10,2017 kuwa Sadifa angefikishwa mahakamani leo.

Alisema kiongozi huyo alikamatwa nyumbani kwake akituhumiwa kwa kuwapa soda wajumbe wa UVCCM kutoka Mkoa wa Kagera kitendo ambacho ni kinyume cha maadili. Kuhanga akithibitisha kukamatwa kwa Sadifa alisema alikamatwa Jumamosi Desemba 9,2017.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: