Zitto Kabwe, Kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo.
Manyara. Diwani wa Gehandu wilayani Hanang mkoani Manyara (ACT -Wazalendo), Mathayo Samhanda amejiuzulu leo Machi 3,2018 .
Baada ya kujiuzulu amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na CCM, akisema anamuunga mkono Rais John Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti katika kuwatumikia wananchi.
Anakuwa diwani wa tatu wa upinzani kujiunga na CCM mkoani Manyara katika kipindi cha mwezi mmoja. Madiwani wengine wa wawili wa Chadema, Nicodemus Tlaghasi wa Bagara mjini Babati; na Emmanuel Axwesso wa Tumati wilayani Mbulu walijiuzulu na kujiunga na CCM.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment