Wakati Robert Mugabe aliondolewa madarakani mwaka uliopita, alikuwa ameitawala Zimbabwe kwa karibu miongo minne.
Swali ni kwa njia gani madikteta wanafanikiwa kubaki madarakani kwa muda mrefu. Mchambuzi James Telly, professor wa masuala ya siasa katika chuo cha Oxford anachanganua mbinu wanazotumia madikteta kubaki madarakani.
Wanawadhibiti vipi watu wa kawaida na kuzuia mapinduzi? Ni vipi wanawazui wapinzani kuwashinda nguvu? Na ni vipi wanavuruga masuala kama uchaguzi kuweza kuendelea kutawala?
Professor James Tilley anachambua baadhi ya mikakati ambayo mara nyingi hutumiwa na madikteta.
Kudhibiti watu
Jambo la kwanza ambalo kila dikteta hufanya ili abaki madarakani ni kuwadhibiti watu. Tunaweza tukafikiria kuhusu njia za kutumia dhuluma, mateso na kuwaua watu lakini pia kuna njia zingine za kutumia dhuluma ambazo huzuia watu kuungana kuipinga serikaki. Rais wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi alipinduliwa mwaka 2011 na kuuawa
Kwenye ulimwengu wa sasa hii mara nyingi humaanisha kudhibiti mitandao.
Mara nyingi serikali ndiyo hufaidika na watu kuwepo kwa wingi katika mitandao.
Serikali ya China imetumia mfumo huu kwa njia kubwa.
Kudhibiti wapinzani
Ni madikteta wachache hupinduliwa kwa njia ya maandamano. Hatua ya pili kila dikteta anachukua ili kubaki madarakani si kukandamiza watu bali kudhibiti watu wachache wenye ushawishi.
Ili dikteta kubaki madarakani watu ambao wanaweza kuwa wapinzani ni lazima wafurahishwe siku zote.
"Kwa mfano nchini Korea Kaskazini, watu muhimu ni majenerali wa jeshi. Watu wachache wa familia na watu wenye vyeo vya juu serikalini huwa ni wale husimamia masuala ya fedha na hao ni kati ya watu wachache hadi mamia ya watu." Anasema Bruce Bueno de Mesquita profesa wa masuala ya siasa katika chuo cha New York. Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un
Sasa uzalendo wa watu hawa unaweza kununuliwa. Hii inamaanisha kutenga pesa kutoka kwa kodi au kutokana na mauzo ya mafuta ambazo zingeweza kutumiwa kwa huduma kwa watu kama mahospitali, kuwazawadi watu wachache kwa magari mengi na makasri.
Madikteta pia hufanya uchaguzi
Madikteta mara nyingine wana mikakati chungu nzima ya kusalia madarakani kama vile kuwadhibiti mahasimu wa kisiasa pamoja na wafuasi wao.
Mbinu ya tatu katika orodha ya kuendelea kutawala ni ya kustaajabisha mno, inajulikana kama ''uchaguzi''.
Mataifa mengi sasa yana uchaguzi mkuu, lakini mara nyingi madikteta huiba kura.
Leo hii, wizi wa kura una mbinu kali sana na ya kisasa, badala ya ile ya zamani ya kujaza makaratasi ya ziada ndani ya masanduku ya kupigia kura. Dkt Brian Klaas, ni mtafiti katika Chuo kimoja kikuu cha Uchumi Jijini London: Obiang Nguema ndiye kiongozi ameongoza kwa miaka mingi zaidi barani Afrika
"Chaguzi nyingi duniani, huwahusisha viongozi wa kiimla ambao mara nyingi, wanawazuia wapinzani wao wakuu wasigombee kiti cha urais kwa kutumia mbinu potovu za kisheria. Mfano mzuri ni uchaguzi mkuu wa Madagascar wa mwaka 2006, ambapo kiongozi wa upinzani alitakiwa kufika mwenyewe katika tume ya uchaguzi mkuu kujiandikisha kibinafsi, (wakati huo alikuwa uhamishoni nje ya nchi).
Ndege yake ilizuiwa kutua mara tu ilipokuwa imabakisha dakika kumi hivi itue kwa kufunga viwanja vya ndege.
Motisha ya kukaa madarakani
Hadi sasa, mbinu za madikteta za kusalia madarakani, sio ngumu hata kidogo. Kuchunguza na kudhibiti raia ambao ndio wapigaji kura, kuwalipa mlungula, baadhi ya watu mashuhuri miongoni mwao na kutumia uchaguzi mkuu kuonyesha tu wana nguvu ya kusalia mamlakani.
Mara tu baada ya watawala hao wa kiimla wanapotawala kwa miaka michache na kubaini mbinu ya kijanja ya kuendelea kukwamilia madaraka, wanakita mizizi na kuwa vigumu mno kuwang`oa uongozini.BBC
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment