BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RUFAA YA MBUNGE JOSEPH MBILINYI, MASONGA YATUA MAHAKAMA KUU KANDA YA MBEYA


Mbeya. Rufaa ya kupinga hukumu ya kifungo cha miezi mitano jela iliyotolewa kwa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga imewasilisha Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya.

Akizungumza na MCL Digital leo Machi 1, 2018 mmoja wa mawakili wa Sugu, Faraji Mangula amesema tayari maombi ya rufaa yao yamepokewa leo mchana na kupewa kumbukumbu namba 29/2018.

“Tayari rufaa yetu imeshapokewa Mahakama Kuu (Mbeya) na tunachosubiri ni kupangiwa tarehe ya kuanza kusikiliza tu, ila tunachoshukuru watu wa Mahakama hii wapo vizuri kushughulikia suala hili,” amesema Mangula.

Mbali na kukataa rufaa hiyo, lakini pia mawakili hao wanakusudia kuomba dhamana kwa wateja wao ili waweze kuwa nje katika kipindi ambacho wanakuwa wanasikiliza rufaa yao.

Sugu na Masonga walihukumiwa baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli. Wawili hao walitoa kauli hiyo Desemba 30 mwaka jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: