BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR (SMZ) YATAKIWA KUONGEZA NGUVU


Serikali ya Zanzibar imetakiwa kutoa kipaumbele kwa shughuli zinazoendeshwa katika kituo cha kutengenezea vifaa vya umeme wa jua cha ‘Barefoot’ kilichopo Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Akizungumza na waandishi wa habari kituoni hapo, Mratibu mkaazi wa ‘Barefoot Collage’ nchini Pendo Yaredi Sambayi alisema mradi huo uliolenga kusaidia maendeleo ya jamii kupitia wanawake wa vijijini unahitaji msukumo ili chuo hicho kiweze kuendelea.

Alisema katika utekelezaji wa kazi zake chuo hicho kinatoa mafunzo ya kutengeneza vifaa vya umeme wa jua na kusimamia uunganishaji wa vifaa hivyo kwa wananchi wa vijiji ambavyo havijafikiwa na huduma ya umeme kwa lengo la kuharakisha maendeleo ya jamii.

Alisema kikawaida chuo hicho kinatakiwa kutoa wahitimu mara mbili kwa mwaka lakini kimeshindwa kufanya hivyo kutokana na kukosekana kwa fedha kutoka serikalini jambo hilo limeshindikana na kutishia maendeleo ya mradi huo.

“Wahitimu wa mwisho walimaliza mwezi April mwaka jana (2017) ambapo wanawake 9 walihitimu baada ya wenzao 11 kuhitimu mnamo mwaka mwaka 2016 jambo ambalo ni kinyume na utaratibu unaotakiwa wa kutoa wahitimu kila baada ya miezi mitano”, alieleza pendo.

Hata hivy aliipongeza serikali ya Zanzibar na ya India kwa kufikiria kuanzisha mradi huo ambao umesaidia kubadilisha maisha ya baadhi ya wanawake wa vijiji vinavyohusika ma utekelezaji wa mradi huu.

“Mradi huu ni miongoni mwa matokeo ya ziara ya Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein alipotembelea nchini india na kutembezwa katika miradi ya huo cha Barefoot ndipo alipoiomba serikali ya nchi hiyo ije kutekeleza mradi huu hapa nchini kwa makubaliano maalum”, alieleza Mratibu huyo.

Aliyataja miongoni mwa makubaliano ahyo kuwa ni pamoja na SMZ kugharmia mafunzo kwa wanawake hao na upatikanaji wao huku serikali ya india kuwezesha ujenzi wa kituo hicho na safari za mafunzo nchini india za wakufunzi miongoni mwa wahitimu 11 wa kituo hicho.

Aidha katika kuendeleza malengo ya mradi huo Pendo alieleza kuwa wameamua kutoa mafunzo ya ushonaji nguo za aina mbali mbali, ufugaji nyuki na kilimo chenye kuzingatia utunzaji wa mazingira ambayo wahitimu wanatakiwa kwenda kuyafanyia kazi pindi wanaporudi katika vijiji vyao.

Akielezea mafanikio ya kituo hicho mratibu huyo alieleza kuwa idadi ya vijiji wanavyovihudumia imeongezeka na kufikia vinane Unguja na Pemba ambapo zaidi ya nyumba 1,000 zimeshafungwa vifaa vya umeme huo.

“Kwa sasa tupo katika vijiji 6 unguja na 2 pemba ambap kinamama wapaooondoka hapa kila mmoja hupatiwa vifaa vya umeme jua 50 ili akaviunganishe na kuwavungia watu 50 na kuwasimamia katika malipo ambayo ni madogo kulingana na vifaa vyenyewe lakini pia fedha hizo huwa ni mali yao kama kikundi au jamii”, alieleza.

Nae kiopngozi wa timu ya kijamii wa kituo hicho aboubakar khalid alieleza licha ya kufanikiwa kuwa na wahitimu 20 hadi kufikia 2017, bado chuo hicho kinakabiliwa na uhaba wa fedha za kuendeshea mafunzo, vifaa vya kufanyia kazi baada ya masomo na ugumu wa kuwapata wanafuzi kutokana na sababu mbali mbali.

“Mradi huu umelenga kuwawezesha wanawake hasa wale wa vijijini ambao hawakusoma au wana elimu ndogo ambao wana umri kati ya miaka 35 na 55, hivyo baadhi ya wakati inakuwa ngumu kuwapata ili waweze kuhudhuria mafunzo kutokana na kutoruhusiwa na waume au jamaa zao”, alieleza Khalid.

Alisema ugumu wa waume na jamaa za wanawake wanaotamani kujiunga na masomo hayo unatokana na mwanafunzi kutakiwa kubakia chuoni kwa muda wa miezi mitano bila ya kuondoka jambo ambalo linakuwa gumu.

Akizungumzia mafunzo ya ufugaji nyuki yanayotolewa na kituo hicho mratibu wa ufugaji nyuki Zanzibar hassan faraji ali alisema mafunzo hayo yanaenda sambamba na mafunzo ya utunzaji wa mazingira ili kurahisisha upatikanaji wa mavuno mengi.

“Tumeamua kuliingiza somo hili ili kuwafanya wahitimu wetu wawe na ujuzi tofauti tofauti utakaowasaidia kuendeleza maisha yao kwani licha ya kupatiwa nyenzo za kuanzishia miradi yao pia tunawapatia ujuzi wa kutafuta masoko ya bidhaa wanazozalisha”, alifafanua.

Kituo hicho ambacho ni sehemu ya miradi ya chuo cha Barefoot unaotekelezwa katika nchi mbali mbali duniani kwa lengo la kueneza matumizi ya nishati mbadala kama njia ya kutunza mazingira na kuwawezesha wanawake ulizinduliwa na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein miaka mitano iliyopita.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: