'UKARIMU' WA KABILA HILI, MGENI WA KIUME HUPEWA MKE WA KULALA NAYE USIKU KUCHA
Na Geofrey Chambua
Wakati dunia nzima ikipambana kuzuia ongezeko la maambukizi ya magonjwa ya ngono kama UKIMWI, Kaswende, Gonorea na magonjwa mengine yanayoshabihiana, hii ni tofauti kabisa na kabila la OVAHIMBA ambalo hadi karne hii ya 21 bado wanatamaduni hatari kwa afya zao.
Kabila la OVAHIMBA ambalo linapatikana kaskazini mwa Namibia katika mikoa ya Kunene na Omusati, bado wanautamaduni wa kuwapokea au kuwakaribisha wageni wa kiume kwa kufanya mapenzi wakiamini kuwa hiyo ndiyo heshima anayostahiri mgeni.
Imeelezwa kuwa mgeni anapowasili kwa siku ya kwanza kama ilivyokawaida huandaliwa chumba na kisha kumteua mwanamke/binti ambaye hajaolewa kwenye familia kulala na mgeni kitanda kimoja kwa siku ya kwanza.
Na kama kwenye familia aliyofikia mgeni hakuna mwanamke ambaye hajaolewa basi wanaume kwenye familia hiyo hupiga kura ili mmoja wao kumuachia mgeni chumba chake alale na mkewe.
Kama mwanaume huyo nyumba yake itakuwa na chumba kimoja na sebule basi atamuachia mkewe alale na mgeni chumbani kwake.
Kwa maelezo ya makala iliyochapishwa na mtandao wa shirika la habari la AP, imeelezwa kuwa wanawake huwa hawana njia ya kukataa maamuzi hivyo moja kwa moja hutii maamuzi ya wanaume kwenye jamii yao.
Asubuhi mwanamke ambaye amelala na mgeni hukaguliwa kama alishiriki tendo la ndoa na kama hakushiriki huongezewa usiku mwingine.
Kwa wageni wa kike hao huachwa walale na watoto na huwa hawafanyiwi chochote.
Kabila la Ovahimba wanaamini kuwa mwanaume yeyote hutembea na bahati, hivyo kwa kulala na mwanamke aliyekwenye familia yao huongeza bahati.
Kwa sensa ya mwaka 2010 kabila hilo lilikuwa na watu 50,000 na tayari serikali nchini Namibia imepanga namna ya kuiokoa jamii hiyo ya wafugaji ambayo inaishi karibia na jangwa la Namib.
0 comments:
Post a Comment