BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHUKI YA WAZUNGU ILIVYOMWONDOA MWANAHARAKATI MWEUSI DR MARTIN LUTHER KING DUNIANI KWA KUMPIGA RISASI

Huenda maisha tunayaona jana na leo lakini si rahisi kuyaona kesho.

Na Geofrey Chambua.
Marehemu Mbarak Mwinshehe aliimba ukiishi kwa kupiga mayoye utapoteza muda mwingi kukumbukwa kesho ni vyema ukayaishi maneno kwa vitendo vyako ili kesho ukumbukwe maana utakumbukwa si kwa magari, majumba wala hela ulizoacha bali ni jinsi gani Maisha yako yaliwagusa watu.

Jana ilikua ni miaka 50 tangu kuuliwa kwa kupigwa risasi kwa Mmarekani mweusi Martin Luther na kundi la wazungu waliochukia harakati zake za kupigania haki za weusi.

Aliuwawa tarehe 04/04/1968. Anakumbukwa kwa hotuba yake maarufu ya I have a dream yaani nina ndoto.

Martin ni miongoni mwa wanaharakati wengi walioishi kwa muda mchache sana Duniani ila wameacha kasumba/legacy kubwa sana Duniani. 


Pamoja na kuwa inasemakana aliuwawa kwa maagizo ya FBI chini ya Murugenzi katili John Edgar Hoover miaka 50 iliyopita lakini amebakia kuwa mtu mashuhuri na maarufu sana na unaweza ukasema amefariki jana tu.

Kuna mkanganyiko mkubwa juu ya akina Martin Luther kwa kuwa wote wawili wana majina yanayoelekeana sana mwanzo na mwisho. 


Hawa ni Martin Luther wa ujerumani aliyekuwa mwanaharakati wa kidini aliyekuwa mwanamatengenezo ambaye aliwezesha kuzaliwa kwa dhehebu la Lutherani duniani na wa pili ni Martin Luther king Jr wa marekani ambaye alikuwa ni kiongozi wa kidini na kiongozi wa harakati za kumkomboa mtu mweusi marekani.

Hivyo tofauti kubwa ya watu hawa ni mataifa mmoja ni wa marekani na mwingine ni wa ujerumani. Na mmoja ni mwenye asili ya afrika(Martin Luther king Jr) na mwingine ni mjerumani mweupe(Martin Luther).

Katika makala haya nitamuongelea Martin Luther king Jr wa marekani ambaye alikuwa ni kiongozi wa kidini na kiongozi wa harakati za kumkomboa mtu mweusi marekani kutokana na ubaguzi wa rangi.


Makala hii inajikita katika kuangalia chimbuko la yeye kuwa kiongozi, sababu za uongozi kuwa imara, udhaifu katika uongozi wake na mafunzo kwa viongozi wengine.

Martin Luther King Jr ni moja ya wanaharakati wakubwa sana nchini Marekani hasa ktk kupigania haki za waamerika Weusi ktk karne ya 20.

Akimtambulisha kama gwiji wa maadili wa karne ya 20, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuwa alijitoa uhai wake akitetea usawa, haki na mabadiliko ya kijamii bila ghasia na alitwa tuzo maaru ya amani (Nobel) mnamo mwaka 1978

Bwana Guterres anasema miongo mitano hata baada ya kifo chake, bado Martin Luther King Jr. ameendelea kuwa na ushawishi mkubwa kwa watu wengi kote ulimwenguni, hususan wale wanaosaka haki za binadamu, wanaobaguliwa na kukandamizwa.

Alizaliwa Januari 15,1929 huko Atlanta ,Georgia nchini Marekani .Wazazi wake walimlea ktk maadili ya Dini ya kikristo na inasemekana walikuwa viongozi wa Dhehebu la Baptist.

Nje ya kuwa mwanaharakati wa masuala ya Haki na Usawa kwa wamarekani weusi Luther alikuwa ni Mhubiri wa Dhehebu la Baptist.

Kwa hiyo kuwa mwanaharakati wa haki za Binadamu na kuwa mhubiri ni jambo la kawaida na Mwenyezi Mungu hakatazi popote pale ktk maandiko yake matakatifu ,kwanza Mungu mwenyewe anapenda haki anachukia dhuluma,manyanyaso,Ubaguzi wa namna yeyote ile na yeye ndiye mwanzilishi na Msingi wa haki chamsingi harakati zako zisivuke mipaka ya neno lake na Taratibu za nchi yako husika.

Alijibebea umaarufu mkubwa sana kwenye Hotuba nzito sana inayojulikana kama "I HAVE A DREAM" Aliyoitoa Agosti 28,1963 mjini Newyork ktk Mnara wa Kumbukumbu wa Rais Abraham Lincoln.


Katika hotuba hiyo alielezea matumaini Makubwa kwa watu weusi akisema ipo siku wamarekani weusi wataupata Uhuru na Usawa ktk Ardhi ya Amerika.

Katika hotuba hiyo watu takribani 200000 walihudhuria kumsikiliza mwanaharakati huyu wa kupinga ubaguzi ktk Amerika na Duniani kote. Aliuchukia ubaguzi wa Kirangi,Kidini,Kipato n.k 


 Wakati wa karne ya 20 huko Marekani kuliibuka ubaguzi mkubwa wa Kirangi kwenye Taasisi za Kielimu ,kiafya na kidini ,vyombo vya usafiri ,Kwenye kumbi za Starehe ,Kwenye Ofisi za Umma ,Kwenye mashamba,Kwenye Viwanda, Kwenye maduka,Kwenye masoko,n.k waamerika weusi walinyanyapaliwa sana

Ilikuwa ukimuona mzungu na umekaa kwenye seat unampisha ikiwa gari limejaa,ukigoma unaadhibiwa vibaya sana,mwaafrika ulikuwa huruhusiwi kula hoteli moja na mzungu ,Mwafrika hakuruhusiwa kusoma Shule na Mzungu au mtoto wa kizungu.


Ilikuwa hairuhusiwi mzungu na mwafrika kuoana na lilikuwa ni kosa kubwa sana kufanya hivyo n.k .Hivyo kulikuwa na hotel,hospitali ,maeneo ya burudani ,makanisa n.k ya wazungu na waafrika .

Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya akina Marcus Garvey ,William Dubois ,Malcolm X walisimama kidete kutoa hotuba za kulaani vikali vitendo vibaya vya kibaguzi vilivyokuwa vinafanywa na wazungu kwa kutumia majarida,vitabu ,kuandika mapendekezo ya sheria zinazolinda watu weusi dhidi ya wazungu katika Bunge la Marekani.


Walitumia Redio na Televisheni kupinga ubaguzi wa Rangi,walitumia mbinu ya maandamano kuamusha hisia za Tabaka baguliwa (Waamerika weusi) n.k .Watu hawa walifanya kazi kubwa sana ya kupinga ubaguzi uliofanywa na wazungu.

William Dubous na wanaharakati wengine walianzisha mpango uliojulikana kama "BACK MOVEMENT " Ukimaanisha kuwa sasa waafrika warudi kwao wakaijenge Afrika yao ,wengi walirudi na wengine wengi pia walibaki wakiamini kuwa ipo siku wangepata Uhuru na Usawa katika Ardhi ya Amerika.


William Dubous alionyesha mfano kwa kuhama Marekani na kuja kuishi Afrika ktk nchi ya Ghana mjini Accra.

Martin Luther King Jr ni moja ya watu walioamini kuwa ukombozi utapatikana huko huko Marekani na hakuamini katika kuikimbia Marekani .Funzo tunalopata haki haipiganiwi ukiwa ng'ambo Bali ukiwa ktk nchi yako.Waswahili wanasema fimbo ya mbali haiuwi nyoka.

Luther aliendelea kuwapigania waafrika huko huko Marekani na kujitwalia Tuzo kadhaa za Amani (Nobel Prizes) baada ya kuutsmbua mchango wake ktk kuwapigania waamerika weusi .

Harakati za kupigania Uhuru na Usawa kwa wamarekani weusi zilikuwa ngumu sana kwani kulikuwa na kikundi cha Siri kilichojulikana kama Ku Klux Klan au Kuklux Clan kilichoundwa na wazungu ili kufifisha harakati za wamarekani weusi kudai Uhuru na usawa huko Marekani. Kikundi hiki kilikuwa hatari sana kwani kilikuwa kinawalenga viongozi wa harakati ili kiwaue .

Martin Luther king Jr aliuwa kwa kupigwa Risasi Hapo Aprili 4,1968. Kijana aliyetekeleza unyama huu alikuwa ni wa kizungu alijulikana kwa jina la James Earl Ray huko mjini Memphis, jimbo la Tennessee.

Martin Luther king Jr atakumbukwa kwa mbinu zake za kudai haki ,Uhuru na Usawa miongoni mwa wazungu na watu wa jamii ya kiafrika .Alidai haki ,Uhuru na usawa bila kuofia kulipa damu yake ktk harakati za ukombozi .

Martin Luther king Jr alituma ujumbe mzito Barani Afrika,Amerika ya kusini na Asia kuwa Uhuru ,Haki na Usawa unapaswa kuheshimiwa kwa Binadamu wote bila kujali wewe ni wa Rangi gani ,kipato gani,Dini gani ,n.k

Martin Luther king Jr atakumbukwa sana hasa ktk hotuba yake maarufu ya "I HAVE A DREAM" Akimaanisha "Nina ndoto" ambayo ilitoa unabii mkubwa sana wa Uhuru, haki na Usawa na hatimaye Dunia ilishuhudia Marekani ikiongozwa na mwamerika mweusi mh.


Barack Obama wakati miaka ya nyuma ilikuwa ni marufuku kwa wamarekani weusi kushiriki ktk medani za kisiasa na hata kupiga kura hawakuruhusiwa.

Harakati za Martine Luther umeleta mafanikio makubwa ndani ya
Amerika ya Leo. 


Kuna tofauti sana na Amerika ya Jana hasa katika kuutazama usawa kati ya Marekani mweusi na mmarekani mweupe. Hivyo kupitia history hii niwaambie wanaharakati wetu kuwa kuna siku matunda ya kazi yao yataonekana
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: