BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS MAGUFULI HANA HURUMA, ATAKA POLISI KUKAMATA KIJIJI KIZIMA CHENYE MASHAMBA YA BANGI


Arusha. Rais John Magufuli ameagiza askari kuwakamata wazee, wanawake, vijana na watoto wa maeneo yanapobainika mashamba ya bangi akieleza kuwa wakikamatwa watasema ukweli na watazifyeka wenyewe.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Aprili 7 wakati akizungumza na wakazi wa Arusha Uwanja wa Sheikh Amri Abeid baada ya kuzindua kituo cha polisi na nyumba 31 za polisi.

“Sitaki Jeshi la Polisi litumike kufyeka bangi, kwa nini mkafyeke bangi? Tumieni intelijensia yenu mkakae pale kijijini na mtajua nani anakwenda kukagua mashamba hayo. Nyie shikeni wote katika hicho kijiji, kamateni wote, wazee, wanawake hata watoto shika, ndipo watasema ukweli,” amesema. Rais amesema wanaolima bangi wakikamatwa ndio wanaotakiwa kuzifyeka.

Sirro asema askari 458 walifukuzwa kazi kwa utovu wa nidhamu
Dar es Salaam. Jumla ya maofisa wa Jeshi la Polisi wapatao 458 wamefukuzwa kazi kutokana na utovu wa nidhamu kuanzia mwaka 2015 hadi Machi mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro alipokuwa akizungumza mbele ya Rais John Magufuli wakati wa uzinduzi wa nyumba 31 za Polisi na ufunguzi wa kituo cha Polisi cha Utalii na Kidiplomasia jijini Arusha.

Sirro amesema kazi ya Jeshi la Polisi ni kurekebisha mienendo ya wananchi, hivyo kabla hawajawaelimisha wananchi wanapaswa kuwa na mienendo mizuri wao kwanza.

Amefafanua kwa kulitambua hilo ndiyo maana askari waliokwenda kinyume na azma hiyo walichukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi, ambapo kwa mwaka 2015, 198 walifukuzwa kazi.

Amesema kwa mwaka 2016 walifukuzwa askari 165, 2017 (81) na kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu wamefukuzwa askari 14. “Hatuna muhali kuwachukulia hatua askari wanaokiuka utaratibu na nidhamu ya utendaji katika Jeshi la Polisi,” amesema IGP Sirro.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: