BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBUNGE SUGU BADO ANAENDELEA KUNG'ANG'ANIA MAMBO YA GEREZANI


Dodoma. Mbunge wa Mbeya Mjini, (Chadema) Joseph Mbilinyi (Sugu) ameitaka Serikali kuwasaidia askari magereza wanaostaafu kulipwa mafao bila ya usumbufu kwani wanapostafu husubiri hadi zaidi ya miaka miwili.

Akizungumza leo Juni 4 bungeni, Sugu amesema Serikali huwasumbua askari hao bila sababu za msingi wakati wanafanya kazi ngumu ya kuwatunza wahalifu.

“Mheshimiwa spika, serikali inasema kuhusu askari hawa ambao wamekuwa wakisumbuliwa kutolipwa stahiki zao baada ya kustaafu wakati polisi wanaotukamata na kutupiga wanalipwa mapema lakini wahalifu wote wanarundikwa magereza kwa hiyo hawa wanakuwa na kazi ngumu,” amesema Sugu.

Spika wa Bunge Job Ndugai amesema kuwa swali hilo licha ya kuwa ni refu lakini ameamua kuliacha lijibiwe kwani limeulizwa na mtu mzoefu kuliko maswali mengine yanayoulizwa kwa ubabaishaji.

Akijibu swali hilo na swali la msingi kutoka kwa mbuge wa Viti Maalum Lucy Mlowe (Chadema), Naibu Waziri wa Fedha Dk Ashatu Kijaji amesema Serikali inalipa mafao kwa wastaafu wote bila ya upendeleo na kuwa katika kipindi cha hivi karibuni, zililipwa jumla ya Sh 282 bilioni kwa wastaafu mbalimbali. 


Naibu waziri amewaondoa hofu pia watumishi wote walioajiriwa katika miaka ya 1980 kupitia Serikali Kuu lakini wakati ule hapakuwa na makato ya mfuko wa kijamii.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: