BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

POLISI MORO YAITANDIKA MWANZA UNITED CCM KIRUMBA

TIMU ya soka ya Polisi Morogoro imejiweka katika nafasi mzuri ya kurejea ligi kuu Tanzania Bara baada ya kutoa kipigo kikali dhidi ya timu ya Mwanza United ya Jijini Mwanza wakati mfululizo wa michezo ya ligi daraja la kwanza uliofanyikwa kwenye uwanja wa CCM Kilumba kwa bao 4-0.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Jijini Mwanza Kocha Mkuu wa timu hiyo, John Tamba alisema amefurahishwa na matokeo ya ushidi dhidi ya Mwanza United baada ya timu yake kuibuka na kushindi mnono ugenini kuwa lengo lao na mikakati waliojiwekea ya kurejea ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao yanaendelea kuwa mavizuri.

Tamba alisema kuwa vijana wake baada ya kupoteza michezo miwili nyumbani katika uwanja wa Jamhuri kwa sasa wachezaji wana ari ya ushindi na kiu ya kurejea ligi kuu msimu ujao hali ambayo inawafanya wachezaji kucheza kwa kujituma na maarifa zaidi ili kuweza kutimiza malengo ya timu ya Polisi Morogoro ya kurejea ligi kuu ambapo katika harakati hizo amewaomba wadau wa soka kuwaombea dua njema ili kuweza kushinda michezo iliyosalia.

Kocha huyo aliwataja wachezaji waliofunga mabao katika mchezo huo kuwa ni mshambuliaji chipukizi Keneth Emmanuel kupachika bao la kuongoza katika dakika ya 15 kufuatia kazi mzuri ya mshambuliaji Nicolaus Kabipe kabla ya mfungaji kukwamisha mpira kwenye nyavu na kuandika bao la kuongoza.

Katika dakika ya 65 na 70 kiungo mchezeshaji Imani Mapunda wa Polisi Morogoro alionekana kuwa mwiba mchuku kwa mabeki wa timu ya Mwanza United kwa kuwahadaa kwa chenga mara kwa mara baada ya kumtengenezea nafasi mbili mzuri mshambuliaji Nocolaus Kabipe na kufunga bao la mbili na la tatu dhidi ya wapinzani wao.

Baada ya timu ya Mwanza United kuona mambo yanawaendea kombo walifanya mashambulizi ya kustikiza langoni mwa Polisi Morogoro lakini juhudi hizo zilikwamishwa na mlinda mlango wa timu hiyo Saidi Kawambwa ambaye aliondoa hatari zote zilizoelekewa katika lango lake.

Tamba alisema kuwa kalamu ya mabao ya Polisi Morogoro ilihitimishwa na mshambuliaji wao tegemeo Nicolaus Kabipe aliyefunga bao la nne na ushindi kwa timu yake katika dakika ya 82 baada ya kazi mzuri ya nahodha wa timu hiyo Mokili Lambo aliyewapiga chenga mabeki wa Mwanza Unitad kabla ya kutoa pasi ya mwisho kwa mfungaji na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa bao 4-0.

Timu hiyo itatelemka dimbani jumamosi ya wiki hii katika uwanja wa Ally Hassani Mwinyi mkoani Tabora dhidi ya timu ya Rhino FC kabla ya kurejea katika uwanja wake wa nyumbani kumalizia michezo yake miwili ya ligi hiyo ikiwa imecheza michezo ya kushinda nne na kufungwa michezo miwili na katika michezo hiyo imeweza kukusanya pointi 12.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: