BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MASHINDANO YA MEI MOSI KUTUMIA SH 15MIL MORO.

JUMLA ya sh 15Mil zinatarajia kutumika kwa ajili ya gharama za kundesha mashindano ya Mei Mosi yanayoshirikisha zaidi ya michezo sita tofauti ambayo yanafanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Akizungumza na gazeti hili katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Katibu Mkuu wa Kamati ya Michezo ya Mei Mosi Taifa, Award Safari alisema kiasi cha sh 15Mil zinatarajia kutumika ikiwa ni gharama za kuendesha mashindano ya Mei Mosi sambamba na ununuzi wa zawadi kwa washindi mbalimbali ambao wanaoshiriki katika michezo sita tofauti mjini hapa.

Safari alisema kuwa baadhi ya michezo tayari washiriki wake wameanza kushindana ikiwemo mchezo wa mpira wa miguu kwa wanaume, netiboli kwa akinamama na kuvuta kamba wanaume na wanaweke.

Alitaja michezo mingine ambayo bado washiriki wake hawajaanza kushindana kuwa ni draft, mbio ndefu kilometa 15, mbio za baiskeli kilometa 15 na karata ambapo michezo hiyo itashindaniwa wanawake na wanaume.

Aidha Katibu Mkuu huyo alisema kuwa wanamichezo wanaoshiriki michezo hiyo wametoka katika mashirikisho manne ya wanamichezo wafanyakazi katika wizara na idara za serikali, masahirika ya umma, taasisi na makampuni binafsi kutoka mashirisho manne.

Aliyataja mashirikisho hayo kuwa ni Shimiwi, Shimuta, Shimisemita na Bammata ikiwa ni kati ya visheheresho katika maadhimisho ya kusherekea kilele cha Mei Mosi itayofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Pia Safari alisema kuwa mpaka sasa kuna timu 12 za mpira wa miguu zinazoshiriki mashindano hayo huku timu za netiboli 17 zikishiriki na zaidi ya timu za michezo mingine 18 ambazo zinatarajia kushinda kuanzia april 25 ambapo april 23 michezo ya soka, netiboli na kamba zinatarajia kumaliza katika hatua ya makundi na timu zitakazofuzu kuingia robo fainali zitakuwa zimejulikana.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: