BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBUNGE KUWALIPIA FAINI WAFUNGWA NA MAHABUSU MORO.

Na Fatuma Mwampepo, Morogoro.

MBUNGE wa Morogoro mjini kwa tikiti ya chama cha Mapinduzi Abdulaaziz Abood ameahidi kuwalipia faini wafungwa na mahabusu hamsini ili waweze kuachiwa huru baada ya kutembelea gereza la Mahabusu la Mkoa wa Morogoro.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa wakati wa ziara yake ya kikazi mjini hapa Abdulaaziz Abood alisema kuwa ammeamua kufanya hivyo ilikupunguza msongamano wa mahabusu katika gereza hilo ambapo wengi wanatumikia adhabu kwa kushindwa kulipa faini.

Abood alisema kuwa msongamano mkubwa katika gereza hilo la mahabusu mkoani Morogoro linauwezo wa kuhifadhi watu 144 ambapo kwa sasa kuna wafungwa na mahabusu 565 ambapo msongamano huo unatishi kuwepo kwa magonjwa ya milipuko.

Aidha alisema kuwa mahabusu wengi wamelalamika upelelezi wa kesi unaowakabili zimekuwa zikichukua muda mrefu miaka mitano hadi bila ya kusikizwa.

Pia alisema mahabusu na wafungwa katika gereza hilo wamelalamikia kunyimwa nakala za hukumu zao hali iliyowafanya wafungwa wengi kushindwa kukata rufaa kutokana na kutoridhika na mwenendo wa usikilizaji wa kesi zao.

Aidha alisema kuwa gereza hilo linakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo kuchakaa kwa vifaa vya kupikia na uhaba wa maji unaotokana na wingi wa wafungwa na mahabusu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: