KIKWETE APONGEZA JUHUDI ZA MBUNGE KUSAIDIA UJENZI WA BARABARA KWA KUTENGENEZA KIWANGO CHA LAMI MORO.
JK KULIA AMKISIKILIZA MENEJA WA WAKALA WA BARABARA MKOA WA MOROGORO DOROTHY MTENGA WAKATI AKIELEZWA JUU YA MRADI WA BARABARA INAYOJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI YA KILOMETA TATO HUKU MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO KUSINI INOCENT KALOGERIS KUSHOTO AKIJITOLEA KUTENGEZA BARABARA KWA KIWANGO HICHO CHA LAMI KILOMETA TATU INAYOANZIA NJIAPNADA YA MATOMBO MSALABANI HADI NJIAPANDA YA MTOMBOZI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOROGORO VIJIJINI MKOANI HAPA.
RAIS JAKAYA KIKWETE (KATIKATI) KULIA MWENYE SHARTI LA KIJANI MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO KUSINI, INOCENT KALOGERIS NA KUSHOTO MKUU WA MKOA WA MOROGORO JOEL BENDELA KWA PAMOJA WAKIKAGUA DARAJA LA MTO MTOMBOZI LILILOPO KATIKA HALMASHAURI YA MOROGORO VIJIJINI AMBAPO JK ALIFANYA ZIARA YA SIKU TATU MKOANI HAPA.
RAIS Jakaya Kikwete amepongeza juhudi za mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini, Inocent Kalogeris za kutumia zaidi ya sh550 Mil kwa ajili ya kutengeneza barabara yenye umbali wa kilometa tatu kwa kiwango cha lami katika mji mdogo wa Mtamba tarafa ya Matombo katika halmashauri ya Morogoro Vijijini mkoani hapa.
Katika ziara yake ya siku tatu katika mkoa wa Morogoro Rais Kikwete alizundua miradi miwili ya madaraja ya Magogoni na Mtombozi, kukagua mradi miwili ya ujenzi wa barabara inayotengezwa kwa kiwango cha lami yenye umbali wa kilometa tano na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa soko la kisasa la Mtamba.
Meneja wa Wakala wa Barabara mkoa wa Morogoro, Dorothy Mtenga alimweleza Rais Kikwete kuwa katika mradi huo wa barabara wenye umbali wa kilometa tano, wakala wa barabara mkoa huo umetenga kiasi cha sh395 Mil kwa ajili ya kutengeneza kilometa mbili huku mbunge wa jimbo hilo akitengeneza kilometa tatu kwa gharama ya sh550 mil. Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita tano inayoanzia njianda ya Matombo Msalabani hadi njiapanda ya Mtombozi, inajengwa na kampuni ya ujenzi ya TGS Company Limited ya Morogoro.
“Mhe Rais huu mradi tumepanga kutumia kiasi cha sh945 katika kilometa hizo tano ambapo serikali imetenga kiasi cha sh395 na mbunge kiasi cha sh 550Mil lakini gharama za ujenzi kwa pande mbili zinaweza kuongzeka kutokana na mvua ambayo imekuwa ikiharibu baadhi ya sehemu ya barabara hasa katika maeneo ambayo tayari lami imeanza kuwekwa na barabara hii ili iendelee kudumu inatulazima kupata fedha za kutengeneza mifereji ambapo serikali kuu ikituwezesha itakuwa vema ili kulinda barabara hii” alisema Mtenga.
Rais Kikwete akizungumza wakati wa majumuisho katika ziara yake alisema amefurahishwa na kitendo cha mbunge huyo wa jimbo la Morogoro Kusini, Inocent Kalogeris la kujitoa kutengezea barabara yenye umbali wa kilometa tatu na kuipunguzia mzigo serikali jambo ambalo sio la kubeza na kuwataka wanasiasa wengine kuiga mfano huo.
“ni jambo zuri alilofanya mbunge wenu la kujitolea kutengeza barabara yenye umbali wa kilometa tatu sasa tukiwapata watu wa namna hii maendeleo yataendelea kukua kwa kasi hasa maeneo ya vijijini ambapo miundombinu ya barabara imekuwa mibovu” alisema Kikwete.
Katika ziara hiyo aliyoifanya katika halmshauri ya wilaya ya Morogoro Vijijini aliwahutubia wananchi katika mikutano ya hadhara katika vijiji vya Kiroka, Mkuyuni, Mvuha, Kiganila, Mtombozi na Mtamba ambapo aliwataka wananchi kujenga tabia ya kutunza miundombinu ya barabara na madaraja sambamba na kuwafichua watu wanaohujumu miundombinu hiyo kwani inaligharimu taifa fedha nyingi.
Daraja hilo la Mtombozi ambalo limepewa jina la ‘Daraja la Kikwete’ limejengwa kwa gharama ya Sh310 Mil hadi kukamilika kwake, huku darala la chuma la Magogoni likitumia kiasi cha sh128.4 Mil ambapo soko la kisasa la Mtamba likiratajia kutimia kiasi cha sh 85Mil hadi litakapokamilika mwezi Agosti mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment