MASOUD MASASI, MOROGORO.
BONDIA Mohamed Matumla wa Dar es Salaam aliweza kutoa aibu ya ukoo wa matumla baada ya kumchapa bondia Cosmas Cheka wa Morogoro katika pambano la ngumi la kulipwa lisilokuwa la ubingwa lililofanyika januari 1, 2012 uwanja wa Jamhuri mjini mkoani hapa.
Katika ukoo wa familia ya Mzee Matumla, bondia Francis Cheka wa Morogoro ameweza kuwachapa bila huruma mabondia, Rashid Matumla mara tatu huku Cheka akipoteza pambano moja kati ya manne waliyokutana naye Rashid wakati kwa upande wa bondia Hassani Matumla akichapwa mara moja na kunyang’anywa ubingwa wa dunia wa WHO na Cheka.
Mohamedi ambaye ni mtoto wa kwanza wa Rashidi Matumla alifanikiwa kutoa aibu hiyo baada ya kumchapa Cosmas Cheka ambaye ni mdogo wa Francis Cheka kwa pointi 231 dhidi ya 225 katika pambano kali na kusisimu lililojaa ushindani na jazba kutoka kwa wanamasumbwi hao wakati wa pambano hilo lilivuta hisia kwa mashabiki wa mchezo huo.
Kwenye pambano hilo la uzito wa chini wa kilo 57 liliamuliwa na majaji watatu ambapo jaji namba moja, Anthony Ruta alitoa alama 77 kwa Matumla na 74 kwa Cheka huku jaji namba mbili, Agapeter Mnazareth akitoa 76 kwa Matumla wakati kwa Cheka alipata alama 74 na jaji namba tatu, Emmanuel Mlundwa akitoa 77 kwa Matumla na 74 kwa Cheka.
Pambano hilo lilianza kwa Cosmas Cheka kufanya vizuri katika raundi tano ambapo raundi ya kwanza hadi ya tatu aliweza kumthibiti mpinzani wake kwa kumtwanga makonde mazito hali iliyomfanya Matumla kudondoka chini huku raundi ya nne na ya tano akiendelea kufanya vizuri.
Kwa upande wa Mohamed Matumla yeye aliweza kuzinduka katika raundi ya sita hadi ya nane ambapo alitoa upinzani mkali kutokana na kujibu kwa makonde mazito kwa mpinzani wake hali ambayo ilimfanya Cheka kucheza rafu kwa kumpiga kichwa Matumla.
Akizungumzia pambano hilo Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (PST), Emmanuel Mlundwa alisema kuwa katika pambano hilo mabondia wote walicheza vizuri lakini rafu aliyofanya Cheka ya kumpiga kichwa Matumla ilisababisha kupokonywa pointi zilizofanya kukosa ushindi.
“Pambano lilikuwa nzuri lakini kilichomsababishia Cosmas Cheka kukosa ushindi ni ile rafu yake ya kumpiga kichwa Matumla jambo lililochangia kukosa ushindi na isingekuwa hivyo basi ushindi ungeenda kwa cheka kwa kuwa aliweza kutawala kupambano hilo”alisema Mlundwa.
Katika mapambano ya utangulizi bondia Mkulu Katoto alitoka sare na Mohamedi Matimbwa,huku pambano la wanawake Asha Nzoa akimchapa kwa pointi Salma Kihobwa 38-40 ambapo jamila Matimbwa alimchapa kwa ko Mariam Abdallah katika raundi ya pili.
Pambano hilo lilihudhuriwa na mashabiki wengi akiwemo mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera ambaye aliwaongoza mashabiki wa ngumi mkoani hapa.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment