WAKAZI WA KATA YA KIBUNGO JUU WAPANDA MICHEO 337,OOO KATIKA HARAKATI ZA KUHIFADHI MAZINGIRA MILIMA YA URUGURO MOROGORO
Meneja wa Care International Tanzania Dostus Lopa, akizungumza jambo
kwa mmoja wa wakulima ambaye amepata mafunzo ya kilimo mchanganyiko ya
mazao ya biashara na miti ya misitu wakati wa msafara wa kukagua
miradi ya kuhifadhi mazingira na utunzaji wa ardhi katika milima ya
Uluguru eneo la kijiji cha Kibungo halmashauri ya wilaya ya Morogoro
vijijini mkoani hapa.
Meneja wa Care International Tanzania, Dostus Lopa, akifafanua jambo
kwa msafara wa wataalam wa bonde la mto Wami na Ruvu eneo la darasa la
mto Ruvu Kibungo Chini ambapo kumekuwa na uharibifu wa vyanzao vya
maji katika halmashauri ya wilaya ya Morogoro Vijijini mkoani.
JUMLA ya miche mbalimbali ya matunda 337,000 imepandwa katika milima ya Uluguru ikiwa ni harakati za utunzaji wa mazingira na uenezi wa elimu ya matumizi bora ya ardhi ikiwemo ya utunzaji wa vyanzo vya maji katika vijiji vitano vilivyopo kata ya Kibungojuu wilaya ya Morogoro vijijini mkoani Mkoani Morogoro.
Akizungumza na wananchi wa katika kijiji cha Kibungo kwenye mkutano wa hadhara Meneja wa mradi wa Care International Tanzania, Dosteus Lopa alisema kuwa wakulima wa vijiji vitano wamefanikiwa kupanda miche 337,000 ikiwemo ya matunda na miche mingine kwa ajili ya kilimo cha msitu ndani ya kata ya Kibungojuu.
Lopa alisema kuwa miche hiyo imepandwa tangu mwaka 2008 ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa utunzaji wa mazingira wa kuhifadhi vyanzo vya maji na ardhi awamu ya pili katika milima ya Uluguru.
“tumetoa mafunzo kwa wakulima wa vijiji vitano vya kata ya Kibungojuu kikiwemo Dimilo, Kibungo, Lanzi, Nyingwa na Lukenge baada ya kutoa mafunzo ya aina mbalimbali ya utekelezaji wa upandaji miti ya matunda na miti ya mbao, utengezaji wa matuta, uzalishaji wa mazao ya biashara, ufugaji wa mifugo ya kisasa” alisema Lopa.
Lopa alisema mradi huo ulianza mwaka 2008 ambapo jumla ya miche 337,000 imepandwa huku miche 98,000 zaidi ikitarajiwa kupandwaji mara baada ya kuanza kwa mvua za masika katika vijiji vitano vya kata hiyo ya Kibungojuu.
Kwa msimu wa mwaka 2011 wakulima walifanikiwa kupata zaidi ya miti 111,500 kwa aina mlinyaweza 7,458 na mikababu 25,083, mikangazi maji 20,368, mivinje 58,018 na miche ya matunda mchanganyiko 6,588.
Aliitaja aina miche iliyochanganyika ikiwemo ya miti ya matunda na miti ya misitu katika vijiji hivyo kwa mwaka 2011/2012 kuwa ni 110,362 ambapo katika kijiji cha Lanzi miche ni 11,535, Nyingwa 10,200, Kibungo 40,392, Dimilo 43,485 na Lukenge ni miche 4,750.
Katika mradi huo unaendeshwa kwa pamoja na mashirika ya Care International Tanzania na World Wide Fund ulihudhuri na wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishiri wa serikali ya wilaya Morogoro Vijijini na kampuni ya vinywaji baridi ya coca cola makao makuu.
0 comments:
Post a Comment