BUKINA FC YA MOROGORO YAENDELEA KUSUASUA LIGI DARAJA LA KWANZA TANZANIA BARA KUNDI A.
MSHAMBULIAJI WA BUKINA FC, ALEX ATHANAS (MWENYE JEZI YA BLUE)AKIWANI MPIRA DHIDI YA MLINDAMLANGO WA POLISI CENTRE YA DAR ES SALAAM, AKIBIR BABU KUSHOTO NA MLINZI WAKE KULIA, PAUL BARNABAS POLISI WAKATI WA MCHEZO WA LIGI DARAJA LA KWANZA TANZANIA BARA ULIOFANYIKA KWENYE UWANJA WA JAMHURI MKOANI MOROGORO AMBAPO MCHEZO HUO ULIMALIZIKA KWA SULUHU YA BAO 0-0.
KLABU ya soka ya Bukina FC ya mkoani Morogoro imeendelea kusuasua katika ligi daraja la kwanza Tanzania bara mara baada ya kulazimishwa sare na Polisi Centre ya jijini Dar es Salaam kwa suluhu ya bila kufunga kwa 0-0 mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.
Timu hiyo ya Bukina FC ambayo tayari imetelemka dimbani mara nane huku ikiwa imejikusanyia pointi sita kutokana na michezo hiyo imekuwa haionyeshi kiwango kizuri katika ligi hiyo jambo ambalo inawalazimu kushinda michezo mitatu iliyobaki kama wanataka kuingia kucheza hatua ya tisa bora.
Katika mchezo huo timu ya Polisi Centre walishambulia kwa mashambulizi ya kustukiza huku ikiweka ulinzi mkali kwa mlinda mlango wao, Akibir Babu mbinu hiyo ilisaidia washambuliaji wa Bukina kushinda kupenya ngome hiyo na kufanya mchezo huo umalizike bila kufungana mpaka dakika 90 zinamalizika.
Bukina FC inabidi wajilaumu wenye hasa dakika 90 mshambuliaji, Hamis Rashid kupiga shuti hafifu akiwa eneo la hatari na kudakwa na golikipa wa Polisi Centre huku katika dakika tatu za nyongeza washambuliaji, Hamis Kipepe kushindwa kufumania nyavu akiwa ndani ya eneo la hatari kabla ya walinzi kuondoa hatari.
Polisi Centre inaongoza kundi hilo ikiwa imecheza michezo nane na kufanikiwa kushinda michezo minne kutoa sare miwili na kufungwa mmoja na kujisanyajia pointi 14.
0 comments:
Post a Comment