BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

FOUNTAIN GATE ACADEMY YATOA MSAADA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA MGOLOLE ILI KUPUNGUZA BAADHI YA CHANGAMOTO YANAYOWAKABILI MORO.


Mwanafunzi wa shule ya Fountain Gate Academy darasa la pili Kigurunyembe Morogoro, Pili Lukas (4) akimkabidhi ndoo ya sabuni ya unga mtoto, Adrian Chriatian (6) wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mgolole kilichpo kata ya Bigwa baada ya familia ya shule hiyo ya Fountain Gate Academy kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa kituo hicho, wanaoshuhudia tukio hilo kutoka ni Mkurugenzi wa shule hiyo Japhet Makau na kushoto ni mkuu wa kituo hicho cha Mgolole Felista Mwinuka.

Mfanyakazi wa shule ya Fountain Gate Academy Kigurunyembe Manispaa ya Morogoro wakisomba vifaa mbalimbali kutoka kwenye gari muda mfupi kabla ya kukabidhi kwa uongozi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mgolole kilichopo kata ya Bigwa vikiwa na thamani ya sh5Mil mkoani hapa.



SHULE ya Fountain Gate Academy iliyoko Kigurunyembe imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya sh.Mil 5 kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mgolole ikiwa moja ya sehemu ya kukabiliana na matatizo yanayoikabili kituo hicho kilichopo kata ya Bigwa Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa msaada huo Mkuu wa kituo cha Mgolole St .Felista Mwinuka alisema kuwa kituo hicho kwa sasa kinakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo watoto wachanga wenye umri wa mmwezi 1hadi mmoja kukumbwa na ugonjwa wa malaria kutokana na watoto hao kulala pekee yao.

Mwinuka alisema kuwa watoto hao wamekuwa wakikumbwa na ugonjwa wa malaria kutokna na kushindwa kulala katikati ya kitanda licha ya kuwepo kwa wahudumu wa kuwaangalia wakati wa usiku na wanapogeuka kujikuta wakiegemea pembeni mwa chandarua na kung’atwa na mbu wanaosababisha ugonjwa wa malaria.

“Kituo chetu kinakabiliwa na changamoto nyingi lakini kuna changamoto mbili ambazo zimekuwa zikitusumbua sana ikiwemo hii ya watoto wenye umri wa mwezi 1 hadi mwaka mmoja kukumbwa na ugonjwa wa malaria kutokana na kulala pekee yao kitandani na changamoto nyingine ni kukosekana kwa jenereta ambalo lingesaidia kutapa mwanga pindi umeme unapokatika ambapo hali hiyo inapojitokeza husababisha watoto kulia hasa wenye umri wa mwaka mmoja hadi mitatu” alisema Mwinuka.

Naye Mkurugenzi Mkuu Mtandaji wa Fountain Gate Academy, Japhet Makau alisema kuwa msaada huo umetolewa na familia ya shule hiyo ikijumuisha wanafunzi, wazazi, walimu na wakurugenzi ambao wamekusanya kiasi cha sh5Mil na kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya kutoa msaada katika kituo hicho cha kulelea watoto yatima cha Mgolole mkoani hapa.

Makau alitaja baadhi ya msaada waliotoa kuwa ni sukari kilo 100, mchele kilo 100, mafuta ya kupikia lita 40, sabuni ya kufulia katoni 10, juice, nguo, viatu, biskuti, miswaki, dawa ya meno na madaftari vyote vikiwa na jumla ya sh 5Mil.

Hata hivyo alisema kuwa uongozi wa shule hiyo yenye makao makuu jijini Dar es Salaam na tawi mkoani Morogoro walikaa na kuona haja ya kutoa msaada kwa kituo hicho mara baada ya mkurugenzi huyo kufanya ziara ya kukitembelea kituo hicho na kujionea changamoto wanazokabiliana nazo kisha kuitisha kikao cha wazazi, wafanyakazi na walimu wa shule hiyo ambapo walikubaliana kuchanga kiasi hicho cha fedha ili kuweza kuwasaidia ili kujikimu na mahitaji mbalimbali ya kila siku.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: