MBEYA CITY COUNCEL FC YAINGIA TISA BORA KWA KISHINDI LIGI DARAJA LA KWANZA TANZANIA BARA BAADA YA KUITANDIKA SMALL KIDS 4-0 JAMHURI MORO.
Mlinzi wa Small Kids Alfan Mgeni kushoto akichuana na mshambuliaji wa
Mbeya City Councel, Yusuph Abdallah kulia wakati wa mchezo wa kundi B
ligi daraja la kwanza Tanzania bara mchezo uliofanyika uwanja wa
Jamhuri Morogoro ambapo katika mchezo huo Mbeya City Councel ilishinda
bao 4-0.
TIMU ya soka ya Mbeya City Council F.C imeingia hatua ya tisa bora kwa
kishindo baada ya kuitandika Small Kids katika mchezo wa ligi daraja
la kwanza la Tanzania bara kwa kuifunga kwa bao 4-0 katika mchezo
uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Kutokana na ushindi huo Mbeya City Council FC ndiyo wanaoongoza kundi
B kufuatia kumaliza michezo yake na kuibuka kinara kwa kujikusanyia
pointi 22 kutokana na ushindi wa michezo ya kushinda sita kutoa sare
mitatu huku ikiwa haijapoteza mchezo tangu kuanza kwa ligi hiyo.
Kwenye ushindi huo wa timu ya Mbeya City Council F.C mshambuliaji
Ipiana Samson alipachika mabao mawili huku bao la kwanza akifunga
dakika ya 12 baada ya kazi mzuri ya kiungo mshambuliaji, Fidelis
Casto wakati bao lake la pili akifunga dakika 75 kufuaatia kuwazidi
ujanja walinzi wa Small Kids, Alfan Mgeni, Juma Mmbwanaally na Banza
Waziri kabla ya kufunga bao hilo kwa timu yake likiwa ni bao la nne.
Smal Kids walishinda kutumia vema nafasi walizopata kufunga mabao
lakini kikwazo kikubwa kilikuwa kwa walinzi wa Mbeya City Council FC
ikiongozwa na mlinzi wake, Anthony Matogolo ambaye alihakikisha mlinda
mlango wake Tito Sanga hapati heka heka ambazo zingesababisha kuzaa
mabao.
Vijana wa kocha mkuu wa Mbeya City Council FC, Juma Mwambusi
walitawaliwa mchezo huo na kamwe benchi la ufundi la timu ya Small
Kids halitamsahau kiungo mshambuliaji wa Mbeya City Council FC,
Fidelis Casto kufuatia kutengeneza mabao mawili kwa mfungaji, John
Muunga aliyefunga dakika ya 31 huku mwenyewe akifunga bao la tatu
katika dakika ya 68.
Katika kundi hilo B nafasi ya pili na tatu zinawaniwa na timu za
Majimaji, Mlale JKT ya Ruvuma, Polisi ya Iringa, na Tanzania Prisons
ya Mbeya endapo zitafanya vizuri katika michezo yao ya mwisho ya
kumalizia michezo ya kundi hilo.
0 comments:
Post a Comment