MSHAMBULIAJI wa klabu ya soka ya Mbeya City Councel FC, Patrick Mangunguli ameanza tambo baada ya kupachika mabao sita katika michezo ya hatua ya makundi ya ligi daraja la kwanza Tanzania bara na kuwa upachikaji wa mabao atauendeleza kwenye michezo ya hatua ya tisa bora ili timu hiyo iweze kupata moja ya nafasi ya kucheza ligi kuu ya Vodacom kwa msimu wa mwaka 2012/2013.
Patrick Mangunguli amefanikiwa kupachika mabao hayo katika hatua ya michezo ya makundi hivyo kasi hiyo ataiendeleza kwenye michezo ya tisa bora lengo likiwa ni kukisaidia kikosi hicho kinachonolewa na kocha mkuu Juma Mwambusi ili kupata moja ya nafasi kati ya nne ambazo zitacheza ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kwa msimu ujao.
Akizungumza na gazeti hili kwenye uwanja wa jamhuri Morogoro, Mangunguli ambaye amewahi kutamba na klabu ya Moro United miaka ya nyuma alisema kuwa amejiwekea lengo la pekee kama mshambuliaji ya kuhakikisha klabu yake inapata moja ya nafasi ya kucheza ligi kuu ya Vodacom msimu ujao hasa kwa kupachika mabao ya kutosha kwenye hatua ya michezo ya tisa bora hivyo jukumu alilonalo kwa sasa ni kuendeleza kufanya mazoezi ya nguvu yatayomwezesha kuwa fiti ili aendelee kufunga mabao huku timu yake kuibuka na ushindi katika kila mchezo wa hatua hiyo.
“Kwa sasa tunarudi Mbeya bado sijaelewa program za timu baada ya kumalizika kwa michezo ya makundi na timu yetu kuongoza kundi B tukiwa na pointi 22, ila program yangu kama mshambuliaji ni kufanya mazoezi ya nguvu ukiachilia mbali na yale ya mwalimu ili kujiweka fiti kwani hatua ya tisa boara ni ngumu hivyo lazima wachezaji tuendeleze ushikiano wetu nasi washambuliaji tubakie na kazi ya kuachika mabao ila nina imani Vodacom tutacheza” alisema Mangunguli.
Aidha mshambuliaji huyo alisema kuwa timu yao imekuwa ikicheza kitimu zaidi jambo ambalo linampa faraja na kuchangia kupata ushindi huo ambao una kutokana na ushirikiano uliopo kwa wachezaji ndani ya uwanja na uongozi wao hivyo juhudi zao zitawawezesha klabu hiyo ya Mbeya City Councel FC kupata moja ya nafasi ya timu nne ambazo zitaingia na kucheza ligi kuu ya Vodacom msimu kwa msimu wa mwaka 2012/2013.
Klabu hiyo ya Mbeya City Council FC ndiyo iliyoongoza kundi B kufuatia kumaliza michezo yake na kuibuka kinara kwa kujikusanyia pointi 22 kutokana na ushindi wa michezo ya kushinda sita kutoa sare mitatu huku ikiwa haijapoteza mchezo tangu kuanza kwa ligi hiyo.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / MSHAMBULIAJI WA KLABU YA SOKA YA MBEYA CITY COUNCEL FC PATRICK MANGUNGURI AANZA TAMBO BAADA YA KUPACHIKA MABAO SITA LIGI DARAJA LA KWANZA TANZANIA BAR
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment