MUFTI MKUU WA TANZANIA AENDESHA HARAMBEE YA UJENZI WA OFISI YA BAKWATA KILOSA MORO.
Mufti mkuu wa Tanzania Shekhe Issa Bin Shabaan Simba akizindua kwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi mpya ya Bakwata wilaya ya Kilosa katika msikiti mkuu wa Manyema ambapo mufti huyo alikuwa katika ziaya ya siku tau wilayani humo mkoa wa Morogoro.
Mufti mkuu wa Tanzania Shekhe Issa Bin Shabaan Simba aliyekaa katika kiti akifafanua jambo wakati akiongea na waumini wa dini ya kiislam mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi mpya ya Bakwata wilaya ya Kilosa katika msiki mkuu wa Bakwata wa Manyema wilayani huo katika ziara ya siku tatu mkoani Morogoro.
MUFT mkuu wa Tanzania Shekhe Issa Bin Shabaan Simba ameendesha harambee ya ujenzi wa ofisi mpya ya Bakwata ya wilaya Kilosa ambapo jumla ya shilingi 12.8Mil zilipatikana na mifuko ya saruji 146 katika sherehe ya baraza la mauled lilofanyika kitaifa wilayani kilosa Mkoani Morogoro hivi karibuni.
Akizungumza na gazeti hili mjini hapa Shekhe mkuu wa Bakwata wilaya ya Kilosa, Nassoro Milambo alisema kuwa Mufti mkuu wa Tanzania aliendesha harambee hiyo ambapo jumla ya shilingi 12,896,000 Mil sambamba na mifuko ya saruji 146 na bati 100 vilipatikana katika changizo hilo ambalo ukamilikaji wake utasaidia kukamilika kwa ujenzi wa ofisi hiyo ya wilaya ya Kilosa Mkoani hapa.
Milambo alisema kuwa katika changizo hilo zilipatikana jumla ya fedha taslimu sh 1,396,000Mil na ahadi zilikuwa sh11,500,000 ambapo katika ahadi hiyo Waziri wa fedha na uchumi, Mustafa Mkulo ndiye aliyeahidi kutoa kiasi hicho cha sh10Mil kwaajili ya kuwezesha ujenzi huo kuanza hivi karibuni.
Pia alisema kuwa naye mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bebdela naye aliahidi kutoa jumla ya shilingi 1,050,000Mil na Mkuu wa wilaya Kilosa Halima Dendego aliahidi kutoa shilingi 100,000 na Jumuiya ya umoja wa wanawake Bakwata taifa Tanzani (Juwakita) waliahidi kutoa shilingi 100,000 kwaajili ya kuisaidia kukamilika kwa ujenzi huo ambao utaiwezesha wilaya hiyo kupata ofisi mpya ya kisasa.
“Sherehe za maulid kuadhimisha kuzaliwa kwa kiongozi wetu mtume muhamad (S.A.W) yaliyosomwa kitaifa wilayani Kilosa tumefaidika nayo sana kwani kupitia Mufti mkuu wa Tanzania Issa Bin Shabaan Simba aliendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa ofisi mpya ya kisasa ya Bakwata katika wilaya yetu na kupata jumla ya sh 12,896,000Mil tunamshukuru sana Mufti kwa kuendesha zoezi hilo” alisema Milambo.
Aidha Shekhe Milambo aliwataja baadhi ya watu walijitokeza kuchangia ujenzi huo kuwa ni mkazi wa Kilosa mjini Salim Mwakingi aliyetoa ahadi ya sh 100,000 na Idd Mbuke akitoa bati 100 amabpo alibainisha mchangunuo fedha zilizopatikana kwa upande wa wanaume kuwa ni walichanga jumla ya sh 1,271,000Mil na wanawake wakichangia kiasi cha sh 125,000.
Alisema kuwa mifuko ya saruji 146 imetolewa kama ahadi na taasisi ya kiislam ya Bakwata taifa ngazi ya mkoa na wilaya na kubainisha kuwa ofisi ya Bakwata taifa imeahidi kutoa mifuko 100 ya saruji, Bakwata mkoa wa Morogoro mifuko 10, Bakwata wilaya ya Morogoro mjini mifuko 10, Bakwata wilaya ya Mvomero mifuko tano, Bakwata wilaya ya Kilombero mifuko 5, Bakwata wilaya ya Ulanga mifuko mitatu, ofisi ya Bakwata Ngerengere mifuko mitatu naye mkazi wa Kilosa Rajabu Mfaume mifuko 10 na kufanya ahadi hiyo kufikia mifuko ya saruji kuwa 146.
0 comments:
Post a Comment