BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATOTO 300 HUFARIKI DUNIA KILA SAA MOJA KWA UTAPIAMLO.


SAVE The Children limemsihi Waziri Mkuu wa Uingireza kuitisha mkutano nchini London kwa ajili ya kuzungumzia suala la njaa duniani mapema mwaka huu.

Utafiti mpya uliofanyika umebaini kuwepo kwa utapiamlo na kuwa kiini kinachosababisha vifo kwa watoto wapatao milioni 2.6 kila mwaka kinatokana na njaa.

Ripoti kutoka kundi moja la kimatiafa la kutoa misaada la Save the Children, linasema licha ya juhudi za ulimwengu kumaliza njaa utapiamlo unabaki kuwa tatizo kubwa lililopuuzwa ambalo linaathiri robo ya watoto duniani.

Utafiti uliofanywa mwezi Disemba na Januari umebaini kuwa watoto 300 wanakufa kila saa kwa sababu ya utapiamlo.

Kundi hilo limeongezeka kwa bei ya chakula kulazimisha watoto katika nchi nyingi kuacha shule ili kusaidia familia zao kupata fedha kwa ajili ya kujiku na mahitaji mbalimbali.

Katika kesi nyingi, ripoti ilisema utapiamlo haukuwa matokeo pekee ya kutokuwa na chakula cha kutosha, lakini kwa sababu familia haziwezi kumudu kupata chakula bora.

Save the Children linamsihi Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron kufanya mkutano juu ya njaa duniani pembeni ya michezo ya Olympic mwaka 2012 itakayofanyika huko London baadae mwaka huu.

Shirika lilisema asilimia 90 ya watoto wengi wasiojiweza duniani wangeweza kulindwa kutopata utapiamlo kwa kiwango kidogo cha dola bilioni 10 kwa mwaka.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: