Mwimbaji Whitney Houston afariki
Mwimbaji mashuhuri katika miaka ya 80 na 90 Whitney Houston amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 48, kulingana na mwakilishi wa mwanamuziki huyo. Sababu ya kifo chake Jumamosi usiku hakikufahamika mara moja.
Kulingana na ukurasa wake wa mtandao Whitney Houston, ambaye amekuwa akipambana na matumizi ya madawa kwa miaka mingi, aliuza zaidi ya album, nyimbo moja moja yaani single na video zipatazo millioni 170 katika uimbaji wake.
Habari za kifo chake zilienea katika mitandao Jumamosi usiku, kutoka kwa wapenzi wa muziki na watu wengine mashuhuri kama yeye.
Nyimbo za Houston ni pamoja na single saba ambazo zilikwenda moja kwa moja kushika namba moja katika chati za billboard katika miaka ya 1980, ikiwa ni pamoja na "Saving All My Love for You," "How Will I Know," "Greatest Love of All," na "Where Do Broken Hearts Go."
Binti wa mwimbaji Cissy Houston, Whitney alizaliwa August 9, 1963, huko Newark, New Jersey.
0 comments:
Post a Comment