POLISI MORO YAITANDIKA MANYONI FC LIGI DARAJA LA KWANZA TANZANIA BARA JAMHURI MORO.
MSHAMBULIAJI WA POLISI MORO SC, NICOLAUS KABIPE AKICHUANA NA MLINZI WA MANYONI FC NA CHARLES MSUKA WAKATI WA MCHEZO WA LIGI DARAJA LA KWANZA TANZANIA BARA KATIKA UWANJA WA JAMHURI MOROGORO AMBAPO WENYEJI WALIIBUKA NA USHINDI MNONO WA BAO 4-0.
JUMA NDANDA WA KILABU YA POLISI MORO SC KULIA AKICHUANA NA LIMZI WA MANYONI FC YA MKOANI SINGIDA, CHARLES MSUKA WAKATI WA LIGI DARAJA LA KWANZA TANZANIA BARA AMBAPO KATIKA MCHEZO HUO MANYONI FC WALITANDIKWA BAO 4-0 KATIKA JAMHURI MOROGORO.
TIMU ya soka ya Polisi Moro SC imeipigisha kwata Manyoni FC kutoka mkoani Singida katika mchezowa mkali wa ligi daraja la kwanza Tanzania bara hatua ya pili baada ya kuitandikakwa bao 4-0 katika uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.
Katika mchezo huo ambao Manyoni FC walizidi kilaidara hasa katika eneo la kiungo ambapo ilitoa mwanya kwa Polisi Moro SC kutawalaeneo hilo ambao walitengeneza mashambulizi mengi katika lango lao nakusababisha kupoteza mchezo huo ambao kipindi cha kwanza waliruhusu bao moja hukukipindi cha pili wakipachikwa mabao matatu na kufanya mchezo huo kupoteza kwaidadi ya bao 4-0.
Kalamu ya mabao kwa Polisi Moro SC ilifunguliwa namshmabuliaji Juma Maboga dakika ya nane kwa kufunga bao la kuongoza kwa shhitidhaifu lililomsinda golikipa wa Manyoni FC Juma Mustafa kufuatia krosi yaRamadhan Toyoyo na Polisi kwenda mapumziko wakiongoza kwa bao 1-0.
Kuanza kwa kipindi cha pili vijana hao wa kocha mkuuJohn Simkoko waliendelea kulisakama lango la wapinzania wao na katika dakika ya57 kiungo mshambuliaji Juma Liuzio baada ya kazi mzuri ya mshambuliaji NicolausKabipe aliyewalamba chenga walinzi wa Manyoni FC kabla ya kutoa pasi kwamfungaji na kfunga bao hilo la pili.
Mshambuliaji Nicolaus Kabipe katika dakika ya 65alifunga bao baada ya kufanya kazi ya ziada kwa kuwalamba chenga mlinzi waManyoni FC Cherles Msuka kabla ya kumpiga mchenga golikipa Juma Mustafa nakupachika bao la tatu huku bao la nne lilihitimishwa na mshambuliaji ImaniMapunda dakika ya 72 baada ya kugongena vema na mshambuliaji Nicolaus Kabipe.
Timu ya Polisi Morogoro Morogoro imekujikusanyiapointi 12 baada ya kucheza michezo saba wakati Manyoni FC yenyewe ikiwa napointi mbili baada ya kushuka dimbani mara saba kufuatia ilizozipata kutoka kwaAFC ya Arusha na Polisi Morogoro katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo.
0 comments:
Post a Comment