JUMLA ya timu sita zimefuzu kucheza fainali ya ligi ya taifa ngazi ya mkoa wa Morogoro kutafuta bingwa wa mkoa wa Morogoro kwa msimu wa mwaka 2011/2012 baada ya kumalizika kwa michezo ya makundi katika vituo vya Kilosa na Mkambara mkoani hapa.
Akizungumza na gazeti hili Katibu Mkuu Mtendaji wa soka mkoa wa Morogoro (MMRFA) Hamis Semka alisema kuwa jumla ya timu sita zitawania ubingwa wa mkoa wa Morogoro wakati wa michezo ya fainali ya ligi ya taifa ngazi ya mkoa huo kwa msimu wa mwaka 2011/2012 itayoanza kutimua vumbi februari 25 na kumalizika marchi 4 kwenye uwanja wa jamhuri mkoani hapa.
Semka alizitaja timu hizo kuwa ni Mpepo FC ya Kilosa ikiwa na pointi 12, Kaizer Chief Manispaa yenye pointi 10 na The Wailesrs FC ya Kilombero yenye ikiwa na pointi 10 kutoka katika kituo cha Kilosa ambacho kilishirikisha timu saba.
Kwa kituo cha Mkamba Kilombero ni Mkamba Rangers Kilombero ikiwa na pointi 15, Uhuru Rangers Manispaa yenye pointi tisa Docks FC ya Mvomero pointi nane na timu hizo zikitoka kituo cha Mkamba ambacho kilikuwa na timu sita.
Semka alisema kuwa baada ya kupata timu hizo fainali ya ligi ya taifa ya ngazi ya mkoa wa Morogoro michezo ya kuwania ubingwa wa mkoa huo ambopo katika michezo ya ufunguzi itakuwa miwili ambapo mchezo wa kwanza utakuwa timu ya Kaizer Chief dhidi ya Docks FC ukichezwa majira ya saa 8 mchana huku mchezo wa pili ukiwa timu ya Mkamba Rangers ikichuana na The Wailers FC majira ya saa 10:00 jioni michezo yote ikifanyika uwanja wa jamhuri Morogoro.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment