Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood kulia akisalimiana na wachezaji wa timu ya netiboli ya Wenyeviti wakati wa mchezo wa ufunguzi wa club ya netiboli ya CCM ya Abood Netiboli Club dhidi ya Makatibu katika uwanja wa Jamhuri mkoani hapa ambapo katika mchezo huo Makatibu walifanikiwa kuwatandika wapinzani wao kwa vikapu 16-9
Mchezaji wa timu ya netiboli ya Makatibu CCM Adela Mwaka kulia akitafuta mbinu ya kumtoka mchezaji wa Wenyeviti Doloth Mwamsika katikati huku Clara Kapungu akijiandaa kutoa msaada wakati wa mchezo wa ufunguzi wa club ya netiboli ya CCM ya Abood Netiboli Club dhidi ya Makatibu katika uwanja wa Jamhuri mkoani hapa ambapo katika mchezo huo Makatibu walifanikiwa kuwatandika wapinzani wao kwa vikapu 16-9.
MAKATIBU WAWAHENYESHA WENYEVITI KATIKA UZINDUZI WA MCHEZO WA NETIBOLI CHAMA CHA MAPINDUZI
WACHEZAJI wa timu ya mchezo wa netiboli ya Makatibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Morogoro mjini wamewatambia Wenyeviti wa chama hicho katika mchezo wa mkali wa ufunguzi wa timu ya netiboli ya Abood Netiboli Club kwa kuitandika vikapu 16 dhidi ya 9 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.
Dalili za ushindi kwa Makatibu zilianza mapema hasa kutokana na safu ya ulinzi kuwa na kazi ya ziada ya kuwazuia wafungaji wa timuya Wenyeviti ambao walipata wakati mgumu kuweza kutumbukiza vikapu kwenye nyavu.
Wachezaji wa Makatibu Clara Kapungu na Adela Mwaka waliewezesha timu yao kuibuka ushindi wa vikapu 16 huku wachezaji Adela Gibai na Fatuma Sule wa timu ya Wenyeviti wakifanikiwa kufunga vikapu 9 na kufanya mchezo huo kumalizika kwa timu ya Makatibu kuitandika timu ya Wenyeviti vikapu 16-9.
Naye mgeni rasmi katika uzinduzi huo Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Abdullaziz Abood alisema kuwa ili kuwa na timu imara ambayo itakuwa na ushindani katika mashindano ipo haja kwa viongozi wa klabu mpya ya mchezo ya netiboli kuanza mapema kazi ya kuhamasisha wachezaji kupenda mazoezi ambapo itasaidia kupata wachezaji wazuri ambao watateuliwa na kuunda kikosi cha kwanza kwa ajili ya kushiriki mashindano mbalimbali ndani na nje ya mkoa huo Morogoro.
Abood alisema kuwa siri kubwa ya mafanikio ya ushindi katika michezo mbalimbali duniani ni kufanya mazoezi kwa bidii na kujituma hasa kwa wachezaji hivyo wakiwemo viongozi kuwahamasisha wachezaji kufanya mazoezi hapo ndipo chanzo cha kupata mafanikio yanaanzia.
Kwa upande wa Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania wilaya ya Morogoro mjini (UWT), Dotto Maganga alisema lengo la kuanzi kwa klabu hiyo ni kutekeleza kauli mbiu ya kuwa michezo ni furaha, michezo ni afya na kudumisha umoja ndani ya Umoja wa Wanawake Tanzania wilaya ya Morogoro mjini na kwiningeko ikiwemo kuimarisha urafiki baina ya wachezaji kwa wachezaji na viongozi pia ambapo club hiyo inatarajia kutoa wachezaji kujiunga na timu ya netiboli ya CCM makao makuu kwa mashindano ikiwa ni sehemu ya mchanga wao.
0 comments:
Post a Comment